Kumekuwa na kuongezeka lawama za kimataifa za kudhalilisha Quran huko Ulaya. Picha: AFP

Wanachama wa kundi la chuki dhidi ya Uislamu nchini Denmark wamechoma nakala ya Qur'ani tukufu na bendera ya Iraq huku kukiwa na hasira katika ulimwengu wa Kiislamu kutokana na kuvunjiwa heshima kwa Qur'ani iliyoidhinishwa na Sweden.

Kundi la itikadi kali la Danske Patrioter lilichoma kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Copenhagen siku ya Ijumaa.

Pia walibeba bendera yenye kauli mbiu za kuudhi Uislamu, kabla ya kukanyaga bendera ya Iraq na nakala ya Quran chini ya ulinzi wa polisi, kama inavyoonekana kwenye video walizoshiriki kwenye mitandao ya kijamii.

Kundi hilo lilisema lilifanya hivyo kupinga shambulio dhidi ya ubalozi wa Uswidi mjini Baghdad.

Hati za kukamatwa

Mapema siku ya Alhamisi asubuhi, umati wa Wairaki walivamia ubalozi wa Uswidi mjini Baghdad na kuuchoma moto wakipinga tukio la Juni 28 la kuchomwa kwa nakala ya Quran, kitabu kitakatifu cha Uislamu, na Salwan Momika, Mkristo mwenye itikadi kali mzaliwa wa Iraq ambaye sasa anaishi Sweden.

Wakati huo huo, ''Uturuki iitoa ilani ya kukamatwa kwa mwanasiasa mwenye msimamo mkali wa Denmark Rasmus Paludan na washukiwa wengine tisa kwa kuchoma nakala ya Quran mbele ya ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm mwezi Januari,''waziri wa sheria wa Uturuki alisema.

"Ofisi ya mkuu wa mashtaka ya umma imehimiza uchunguzi wa kina kubaini washukiwa na kukusanya taarifa za utambulisho wazi na ushahidi wa vitendo vyao vya uhalifu," Waziri wa Sheria Yilmaz Tunc alisema.

Malalamiko ya kidiplomasia

Uswidi imekuwa ikikabiliwa na msukosuko mkali kutoka kwa mataifa ya Kiislamu kwa kuidhinisha kuvunjiwa heshima kwa Quran.

Siku ya Alhamisi, waziri mkuu wa Iraq aliamuru kufukuzwa kwa balozi wa Uswidi kutoka Iraq na kuondolewa kwa maafisa wa Iraqi kutoka Uswidi.

Kumekuwa na shutuma nyingi na hasira kutoka kwa ulimwengu wa Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Uturuki, Jordan, Palestina, Saudi Arabia, Morocco, Iraq, Iran, Pakistan, Senegal, Morocco, na Mauritania juu ya kuchafuliwa kwa Quran.

Wakati maelfu wakiandamana Pakistan na Iraq, Morocco ilimwita mjumbe wake nchini Uswidi. Katika majibu yake, Iran ilichelewa kumteua balozi mpya nchini Uswidi.

Kwa Waislamu, kuchomwa kwa Quran kunawakilisha kudhalilishwa kwa maandishi matakatifu ya dini yao. Kuchomwa moto kwa Qur'ani siku za nyuma kumezusha maandamano katika ulimwengu wa Kiislamu.

TRT Afrika