Uchomaji wa Qur'an ulizusha maandamano na kulaaniwa duniani kote mapema mwaka huu/ Picha: Kumbukumbu ya AP

Denmark imepitisha sheria inayoharamisha uchomaji wa Qur'ani wenye chuki dhidi ya Uislamu kwa misingi ya "unyanyasaji usiofaa wa maandishi yenye umuhimu mkubwa kwa jumuiya ya kidini inayotambulika."

Kufuatia mjadala mkali kati ya wabunge, mswada huo ulipitishwa kwa kura 94 za ndio na kura 77 zikipinga katika bunge la Denmark lenye wabunge 179.

Mswada huo unafanya kuwa kinyume cha sheria kuchoma, kupasua, au kutoheshimu maandishi matakatifu hadharani au mtandaoni ili kuyasambaza kwa mapana.

Wahalifu wanaweza kupata kifungo cha faini au jela kwa muda wa miaka miwili.

Kumekuwa na matukio ya kuchomwa moto Qur'an mwaka huu.

Saini ya Malkia

Wakati serikali hiyo ya muungano wa vyama vitatu ilipiga kura kuunga mkono mswada huo, hakuna mwanachama wa muungano aliyesimama kujibu ukosoaji wa upinzani wakati wa mjadala bungeni.

Chama cha Social Liberals (Radikale Venstre) kilikuwa chama pekee cha upinzani kupigia kura mswada huo.

Mswada huo uliwasilishwa kwa mara ya kwanza mwezi Agosti lakini baadaye ukarekebishwa kutokana na wasiwasi uliojitokeza ndani ya muungano unaotawala kuhusu uhuru wa kujieleza.

Mswada huo utakuwa sheria kufuatia kusainiwa rasmi na mfalme wa Denmark, Malkia Margre, ambaye anatarajiwa kutia saini baadaye mwezi huu.

Ulinzi bora

Wizara ya Haki ya Denmark ilisema katika taarifa kwamba sheria hiyo inalenga kupambana na "dhihaka za utaratibu," ambazo zinaongeza viwango vya vitisho vya ugaidi nchini Denmark.

"Lazima tulinde usalama wa Denmark na na raia wa Denmark," Waziri wa Sheria Peter Hummelgaard alisema. “Ndio maana ni muhimu kwamba sasa tupate ulinzi bora dhidi ya unajisi wa kimfumo ambao tumeona kwa muda mrefu,” aliongeza.

Mapema mwezi wa Agosti, wanachama wa kundi la Danske Patrioter, au Denmark Patriots, walichoma nakala ya Qur'an mbele ya Ubalozi wa Uturuki huko Copenhagen.

Wahusika waliimba maneno ya kupinga Uislamu wakati wa kitendo hicho cha uchochezi ambacho kilifanywa chini ya ulinzi wa polisi.

Kiburi cha Magharibi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akijibu maandamano ya chuki dhidi ya Uislamu alisema Uturuki haitakubali kamwe kukabiliwa na chokochoko au vitisho.

"Hatimaye tutafundisha mifumo ya Magharibi ya kiburi kwamba kuwatusi Waislamu sio uhuru wa mawazo," Erdogan aliwaambia wanachama wa Chama wa Justice and Development (AK) kupitia ujumbe wa video.

Uturuki "itaonyesha mwitikio wetu kwa njia kali zaidi hadi mapambano madhubuti dhidi ya mashirika ya kigaidi na maadui wa Uislamu, " aliongeza.

TRT Afrika