Iraq imemuamuru balozi wa Sweden kuondoka na kuamua kumuondoa mjumbe wake kutoka Stockholm kwa kuruhusu maandamano ya kuchoma Quran huko.
Waziri Mkuu Mohamed Shia al-Sudani "alimwagiza balozi wa Sweden huko Baghdad kuondoka Iraq," ofisi yake ilisema katika taarifa.
Ilisema uamuzi huo "ulisababishwa na serikali ya Sweden kuruhusu mara kwa mara kuchomwa kwa Quran Tukufu, kudhalilisha utakatifu ya Kiislamu na kuchomwa moto kwa bendera ya Iraq".
TRT Afrika na mashirika ya habari