Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, mwezi Oktoba. / Picha: Reuters  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewataka maofisa wa Israeli kujadili pendekezo la makubaliano katika eneo la Gaza, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema.

Blinken alizungumza na Waziri Benny Gantz na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, kulingana na taarifa hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Blinken "aliipongeza" Israeli kwa pendekezo hilo, kama lilivyobainishwa na Rais wa Marekani Joe Biden, na kwamba, jukumu sasa lilikuwa kwa Hamas ili wakubaliane nalo.

TRT Afrika
Tovuti hii hutumia vidakuzi. Kwa kuendelea kuangalia tovuti hii, unakubaliana na utumizi wa vidakuziSera ya Vidakuzi
Kubali