Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laitisha kikao cha dharura baada ya mashambulizi ya Israeli huko Rafah

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laitisha kikao cha dharura baada ya mashambulizi ya Israeli huko Rafah

Israeli imeua Wapalestina 36,050, wakiwemo watoto na wanawake na kujeruhi wengine 81,026 huku mashambulizi yake dhidi ya Gaza yakiingia siku ya 235.
Miili ya Wapalestina wakiwemo watoto wachanga baada ya kuuwawa na majeshi ya Israeli katika kambi ya Nuseirat, mjini Gaza, Mei 27, 2024. / Picha: AA  

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha kikao cha dharura baada ya shambulio la Israeli katika kambi moja huko katika mji wa Gaza wa Rafah na kuua watu wapatao 45 na kujeruhi wengine 250, huku wengine wakichomwa moto na kukatwa vipande vipande.

Mkutano huo wa ndani unatokana na maombi ya Algeria, ambayo siyo mwanachama wa kudumu wa baraza hilo, wanadiplomasia wamesema.

TRT Afrika