Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan nchini Iran itatoa fursa kwa mataifa yote mawili kuimarisha uhusiano wao. / Picha: Jalada la AA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, anatazamiwa kuanza ziara rasmi nchini Iran Septemba 3, kufuatia mwaliko uliotolewa na waziri mwenzake wa Iran, Hossein Amir Abdollahian, kama ilivyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.

Mataifa yote mawili yatafanya mazungumzo ya ngazi ya juu katika mji mkuu wa Iran wa Tehran.

Majadiliano ya Waziri Fidan na mwenzake wa Iran yanatarajiwa kujumuisha mada mbali mbali, zikiwemo uthabiti wa kikanda, usalama, na matukio yanayoendelea ya kijiografia.

Aidha, ziara hiyo inatoa fursa kwa mataifa yote mawili kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa.

TRT World