Waturuki kupata afueni baada ya kugunduliwa kwa gesi asilia kutoka Black Sea

Waturuki kupata afueni baada ya kugunduliwa kwa gesi asilia kutoka Black Sea

Uturuki inachukua hatua ya kihistoria ili kuweza kujitegema katika uzalishaji wa nishati
Gesi asilia yaBlack sea  itapunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa Türkiye kwenye gesi asilia ya kigeni. Picha(AA)

Uturuki ilianza kutoa gesi asilia kutoka eneo lake la Black Sea siku ya Alhamisi kama sehemu ya mradi wake wa maonyesho ya kupunguza utegemezi wa taifa juu ya uagizaji wa nishati.

‘’Uturuki inachukua hatua ya kihistoria ili kuweza kujitegema katika uzalishaji wa nishati’

Hili lilikuwa ni tamko la Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alikuwepo katika hafla ya uzinduzi wa gesi asilia ya Black sea huko Zonguldak.

Kiongozi wa Uturuki alitangaza kuwa kwa mwaka, kaya zinaweza kutumia gesi asilia bila malipo hadi mita za ujazo 25 kila mwezi.

Akitangaza kwamba eneo hili la gesi asilia hatimaye litasambaza 30% ya mahitaji ya gesi ya Uturuki, Erdogan alisema, "Gesi asilia iliyogunduliwa miaka mitatu tu iliyopita imetumika kwa ustadi na vema kabisa."

Hatua ya pili ya uwanja wa Sakarya inatarajiwa kuongeza uzalishaji wa kila siku kutoka mita za ujazo milioni 10 hadi mita za ujazo milioni 40 ifikapo 2028.

Kulingana na tathmini huru, akiba nzima ya gesi ya taifa hilo ilikadiriwa kuwa mita za ujazo bilioni 710 kufikia mwisho wa 2022, na thamani ya soko ya gesi hiyo ilikiwa takriban dola trilioni moja .

Kwa sasa Uturuki inaagiza gesi yake nyingi kutoka Azerbaijan na Urusi. Ili kupunguza utegemezi wake wa uagizaji wa nishati na kufanya kituo cha gesi cha Filyos kuwa kitovu muhimu cha nishati, Uturuki inatekeleza mkakati unaojumuisha uga wa Sakarya.

Kwa mujibu wa Oguzhan Akyener, msimamizi wa Kituo cha Utafiti wa Mkakati wa Nishati na Kisiasa cha Uturuki, gesi ya kwanza ya Black sea itainua uchumi wa nchi hiyo kwa dola bilioni moja nukta nane(1.8)

Uturuki tayari imetumika kama njia ya kupitisha mabomba makubwa ya gesi ya Kusafirisha gesi katika mataifa ya Ulaya kwa kuwepo kwa miundomsingi katika nchi hiyo kama vile TurkStream katika Black sea.

Rais Recep Tayyip Erdogan atagombea tena kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Mei 14, chini ya mwezi mmoja kutoka sasa baada ya uzinduzi huu.

TRT Afrika