Uturuki inatazamia kuongeza mauzo yake ya nje hadi dola bilioni 265 ifikapo mwisho wa 2023 / Picha: AA 

Uturuki inatazamia kuongeza mauzo yake ya nje hadi dola bilioni 265 ifikapo mwisho wa 2023 "licha ya makadirio mabaya ya kiuchumi duniani," Rais Recep Tayyip Erdogan amesema.

Matamshi ya Erdogan yalikuja Jumamosi alipokuwa akihutubia duru ya thelathini ya kongamano la wasafirishaji nje ya Uturuki na sherehe za tuzo ya mabingwa wa mauzo ya nje jijini Ankara.

"Leo hii, ikiwa tuna bidhaa zilizo na nembo ya 'Made in Türkiye' hata katika maeneo ya mbali zaidi ya dunia, ni wauzaji wetu ambao wana jukumu muhimu zaidi katika hili," alisema. “Licha ya mtazamo hasi wa kiuchumi duniani, tunataka kuongeza mauzo yetu hadi dola bilioni 265 mwishoni mwa mwaka huu na dola bilioni 285 mwaka ujao,” Erdogan aliongeza.

Madhara ya tetemeko 'kupungua'

Rais wa Uturuki pia aligusia athari mbaya kwa uchumi zilizosababishwa na mitetemeko pacha ya Februari 6 yaliyokumba kusini mwa Uturuki.

"Athari mbaya za tetemeko la ardhi kwa uchumi wetu zinapungua siku hadi siku," alisema. "Licha ya maafa ya karne hii, mauzo yetu ya nje yanaendelea kushika kasi."

Erdogan pia alisema kuwa lengo la mauzo ya nje la Uturuki 2028 ni "dola bilioni 400 na zaidi."

"Tunatumai, katika 2023, tutashuhudia watalii wa afya milioni 2 na dola bilioni 3 katika mauzo ya nje kwa pamoja."

TRT Afrika