Uchaguzi wa Uturuki: Uwakilishi wa wanawake katika bunge la Uturuki uko juu zaidi

Uchaguzi wa Uturuki: Uwakilishi wa wanawake katika bunge la Uturuki uko juu zaidi

Wanawake wamepata viti 121 kati ya 600 bungeni
Wabunge wapya wenye umri mdogo zaidi ni wanawake  / Photo: Reuters Archive

Uwakilishi wa wanawake katika bunge la Uturuki utakuwa wa kiwango cha juu zaidi katika historia ya nchi, baada ya uchaguzi wa bunge siku ya Jumapili.

Kulingana na matokeo yasiyo rasmi, wanawake 121 walipata viti katika bunge lenye wabunge 600.

Kiwango cha uwakilishi wa wanawake, kilikuwa asilimia17.1 katika chaguzi zilizopita. Mwaka huu Kilipanda hadi asilimia 20.1.

Mbunge mwenye umri mdogo zaidi wa bunge jipya pia ni mwanamke. Zehranur Aydemir, wa miaka 25, alichaguliwa kama naibu wa Ankara kutoka Chama cha AK na Rumeysa Kadak, 27, akawa Naibu wa chama cha AK Istanbul.

Mamilioni ya wapiga kura wa Uturuki walipiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais ajaye wa nchi hiyo na wabunge.

Duru ya kwanza ya upigaji kura ilimalizika bila mgombea aliyeweza kupata asilimia 50, ya kura kama inavyohtajika, lakini Rais wa sasa Recep Tayyip Erdogan aliongoza, alisema Ahmet Yener, Mkuu wa Baraza Kuu la Uchaguzi, akitaja matokeo yasiyo rasmi.

Idadi ya wapiga kura katika uchaguzi wa Jumapili ilikuwa asilimia 88.92, na waliojitokeza kutoka kwa raia wa Uturuki nje ya nchi walikuwa asilimia 52.69, Yener alisema.

Muungano wa People's Alliance cha Erdogan kimeshinda kura nyingi zaidi bungeni, huku kinyang’anyiro cha urais kikielekea kwenye duru ya pili ya marudio tarehe 28 mwezi Mei.

TRT Afrika