Uturuki inajiandaa kwa uchaguzi muhimu wa kiti cha Meya uliopangwa kufanyika Jumapili, huku awamu ya kampeni ikiwa imepangwa kumalizika Machi 30, siku moja kabla ya uchaguzi.
Wapiga kura kote nchini Uturuki watamchagua meya, mameya wa wilaya, na maafisa wa serikali za mitaa (mukhtars) na vijijini.
Baraza la Uchaguzi la Juu (YSK) limesema ya kwamba uwezo wa kila kituo cha kupigia kura katika Uchaguzi huo utakuwa na wapiga kura 350 katika kila kituo. Huku vyama 35 vya kisiasa vitashiriki katika uchaguzi,
Aidha uamuzi huu unategemea uelewa wa wapiga kura ya kwamba katika kituo kimoja cha kupigia kura watashiriki angalau katika aina mbili za uchaguzi.
Tunachambua kitendawili cha kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki nchini Uturuki
Kufanywa kwa uchaguzi
YSK imeanzisha mfumo unaohakikisha uadilifu wa kura, ukitoka kwenye vituo vya kupigia kura.
Katika kila kituo cha kupigia kura, bodi yenye wanachama watano, ambayo ni pamoja na wawakilishi wa YSK na vyama vikuu vya kisiasa, washirikishwa. Bodi hiyo hukagua vitambulisho vya wapiga kura kuona ikiwa majina yao yamejumuishwa katika orodha ya uchaguzi. Hii inaondoa nafasi ya mtu mmoja kupiga kura mara mbili. Pia husaidia kujenga maridhiano kati ya vyama kuhusu matokeo.
Vyama vya kisiasa, ikiwa ni pamoja na Chama cha Haki na Maendeleo (AK) kinachotawala, na Chama cha Jamhuri (CHP) cha upinzani, vitapeleka maelfu ya waangalizii kwenye vituo hivi vya kupigia kura.
Maelfu ya waangalizi watafuatilia uchaguzi
Kabla ya uchaguzi, vyama huwashirikisha maelfu ya wajitolea, haswa kwa zoezi hili. Wawakilishi hawa wana idhini ya kufuatilia kwa kina masanduku ya kura.
Mbali na wawakilishi wa vyama vya siasa na maafisa wa YSK, mashirika yasiyo ya kiserikali pia yana wachunguzi wao kufuatilia upigaji kura.
Wakati hesabu inapoanza, wajitolea wa vyama vya siasa wapo katika vituo vya kupigia kura kusimamia zoezi hilo. Wanaweza kuhesabu kura, kuchukua picha, na kufikisha habari kwa viongozi wa juu wa chama.
Kile kinachofanya mchakato wa uchaguzi kuwa wazi zaidi ni uwepo wa wachunguzi huru, ikiwa ni pamoja na timu ya wanachama 40 kutoka Baraza la Ulaya na Shirika la Usalama na Ushirikiano huko Ulaya (OSCE), ambao wamekuja kwa mwaliko wa serikali.
Udhibiti wa YSK ulithibitishwa tena mapema mwezi huu, wakati ilikataa ombi la serikali la kudhihirisha data za maeneo ya masanduku ya kura, kabla ya uchaguzi. Aidha upinzani haukukubaliana na YSK kushirikisha maeneo ya masanduku na wizara ya ndani haswa katika wakati muhimu kama huo.
Hii inaonyesha kuwa mamlaka ya uchaguzi wanafanya kazi kwa uhuru bila ushawishi wa kisiasa na kuingiliwa na serikali.
Ili kuepuka sintofahamu wowote, chombo rasmi cha habari cha serikali Anadolu Agency ndicho kilichoorodheshwa kuwa na mamlaka ya kutangaza matokeo ya uchaguzi.