Licha ya kuwepo kwa harakati nyingi za kisiasa na kidiplomasia katika Jiji kuu la Ankara, kuna taasisi maalum iliyoanzishwa kwa ajili ya kutoa taswira tofauti kuhusu Bara la Afrika. Jumba la ‘African House’ lilianzishwa kama mojawapo ya njia za kusherehekea uhusiano wa karibu kati ya Türkiye na Afrika; hatua muhimu iliyotajwa na Mke wa Rais wa Türkiye Emine Erdogan kama “mchango wa busara wa kukuza uimara wa Afrika.”
Ziara ya Bi. Emine Erdogan pamoja na Rais Recep Tayyip katika mataifa mengi ya Afrika ilikuwa kichocheo kikubwa cha kuanzilishwa kwa ‘African House’
Kwa mujibu wa Mshauri wa Rais wa Türkiye na mratibu wa ‘African House’ Tuba Nur Sonmez, msingi wa Jengo hili uliwekwa mara pindi tu baada ya Bi. Ermine Erdogan kuzuru Afrika na kufahama mataifa mengi, kung’amua baadhi ya changamoto na nafasi za ushirikiano zilizopo.
“Lengo hapa ni kuwawezesha wanawake na watoto walioathirika zaidi na hali ngumu ya maisha Afrika(mfano) ugonjwa, njaa, umaskini, ukosefu wa elimu, mizozo (nk). Tuwawezeshe kusudi waweze kujisimamia.” Sonmez aliiambia TRT World huku akiongeza kuwa wanafanya kazi chini ya usimamizi wa Mke wa Rais.
Soko huru na la haki kwa ajili ya Wanawake wa Afrika
“Tunanua bidhaa kutoka kwa watengenezaji-bidhaa wa kike Afrika na kuzikutanisha na mnunuzi kwa bei ifaayo sokoni.”
Lengo kuu hapa ni kuonesha ubora wa bidhaa zenye asili ya Afrika.
“Mapato tunayoyapata yanatumika kwa ajili ya kuwezesha miradi ya Wanawake Afrika.” Sonmez anaongeza.
Yote haya yanafanyika kwa ushirikiano mkubwa wa washikadau tofauti wakiwemo wawakilishi wa Wizara ya masuala ya kigeni, Muungano wa wafanyabiashara MUSIAD, TIKA na Shirika la ndege la Türkiye.
Wageni Tajika
Watu tajika kutokea bara la Afrika hasa Wake za Marais wanazuru sana Türkiye kuja kuangalia tunachokifanya na kuchangia mawazo.
‘Mabalozi kutoka Afrika, wasomi, wafanya-biashara wakuu pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na washikadau muhimu pia katika uendeshaji wa Jumba hili.” Anasema Sonmez.
Watu maarufu waliotembelea ‘African House’ ni pamoja na mjukuu wa Hayati Nelson Mandela Ndileka Mandela, Mke wa Rais wa Angola na Mke wa Rais wa Niger Ana Dias Lourenco na Aissata Issoufou Mahamadou mtawalia.
Mjukuu wa Mandela Ndileka anasema kuwa taifa lake la Afrika Kusini lina mengi ya kujifunza kutoka kwa Türkiye huku Mke wa Rais wa Angola akionesha kuridhishwa kwake kuziona bidhaa za Afrika nchini Türkiye.
“Alisema huku anahisi kama yupo nyumbani baada ya kuziona bidhaa za Afrika. Alifurahi sana kushuhudia mazingira ya KiAfrika hapa.” Sonmez anafichua.
Aidha taasisi hiyo inapania pia kuwaleta pamoja wanafunzi kutoka Afrika kwa kuzuru ‘African House’ kusudi watangamane wenzao kwa wenzao na vile na raia wengine.
“Vipo vitengo vya kufanyia mikutano, kusoma na maktaba iliyo na vitabu kuhusu Africa.”
Pamoja na kwamba jingo hili ‘African House’ linapania kuboresha uhusiano wa Turkiye na Bara hilo; lakini zaidi pia linapania kugusa nyoyo za Wanawake wa Afrika.
“Kwa maneno yake mwenyewe Bi. Emine Erdogan, ‘Urafiki wetu mzuri na wa muda mrefu na Afrika utabaki katika kurasa za historia. Urafiki wetu huu umekuwa kama Bahari kubwa ya Uaminifu’ ,” Sonmez hapa akimnukuu Mke wa Rais Erdogan.