Albares amesisitiza kuwa  "uwepo wa amani katika ukanda huo’’ utasababisha "kuanzishwa kwa dola ya kudumu ya Palestina.’’ /Picha: AA

Mchakato wa Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya si wa kuupuzwa kama "ajenda ndogo za kisiasa za baadhi ya nchi," Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amesema.

"Nilisisitiza kwamba mchakato wa uanachama wa Uturuki ndani ya EU ni muhimu sana kuachiwa kwa ajenda finyu za kisiasa za baadhi ya nchi," Fidan alisema Jumatano katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari akiwa na mwenzake kutoka Uhispania Jose Manuel Albares.

Kusitisha mapigano Gaza

Viongozi wote wawili walizungumzia machafuko yanayoendelea Gaza, na kusisitiza umuhimu wa kuyasitisha.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Jose Manuel Albares Bueno ameelezea umuhimu wa kuchukua hatua na kusitisha mapigano huko Gaza, ambako mashambulizi yalioanza Oktoba mwaka jana, yamepoteza uhai wa wapalestina zaidi ya 31,000, huku nusu yao idadi ya watu wa eneo hilo wakikabiliwa na baa la njaa.

"Tulielezea hitaji la kusitisha mapigano mara moja na ya kudumu. Tulisema kwamba misaada ya kibinadamu isiyo na masharti lazima ifike Gaza,’’ Albares aliuambia mkutano na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Uturuki Hakan Fidan mjini Ankara.

Amani Mashariki ya Kati

Albares aligusia ongezeko kubwa la misaada ya kibinadamu kutoka Uhispania tangu kuanza kwa machafuko hayo, na akatoa wito wa kuachiliwa kwa mateka wote.

Albares alifanya ziara rasmi nchini Uturuki, kwa ajili ya mkutano wa nchi hizo mbili na Fidan, huku uhusiano kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya, maendeleo ya sasa ya kikanda na kimataifa ikiwa ni pamoja na mgogoro wa Gaza na changamoto nyingine katika Mashariki ya Kati, vikitawala mazungumzo hayo.

Alisema kuwa pia walijadili kuhusu "jitihada zipi zitumike kurejesha amani ya Mashariki ya Kati."

“Uhispania inaimarisha sera yake ya amani pamoja na ulimwengu mzima,’’ alisema.

Kuanzishwa kwa dola ya kudumu ya Palestina

Albares alisisitiza kwamba "mustakabali wa amani katika eneo hilo" unahitaji "kuanzishwa kwa taifa la kudumu la Palestina."

"Ni lazima kuanzisha dola ya kudumu ya Palestina," alisema.

Akisisitiza umuhimu wa kudumu kwa amani, waziri huyo wa Uhispania alisema kwamba ‘’usalama, amani na utulivu’’ ni muhimu sio tu kwa Wapalestina na Waisraeli bali pia ‘’kwa mataifa yote ya Mashariki ya Kati.’’

Alisisitiza "jukumu na nafasi kubwa ya Uturuki" katika kutatua "migogoro mikubwa inayoukabili" ulimwengu.

Mgogoro huu umejadiliwa kwa kina na katika hali ya kutafakari wakati wa mkutano baina ya mawaziri wa mambo ya nje, Albares alisema.

TRT Afrika