Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki na Afrika Kusini walijadili masuala ya pande mbili, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa ushirikiano wa ulinzi. Picha: AA

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan siku ya Ijumaa alikutana na mwenzake wa Afrika Kusini Ronald Lamola mjini Johannesburg.

Fidan na Lamola walifanya mazungumzo kama sehemu ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20, kwa mujibu wa vyanzo vya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.

Mkutano huo ulishughulikia uhusiano wa kibiashara baina ya nchi mbili, fursa za uwekezaji wa pande zote, na uwezekano wa ushirikiano katika sekta ya ulinzi.

Majadiliano pia yalijumuisha matukio ya hivi punde katika kesi ya mauaji ya halaiki iliyowasilishwa dhidi ya Israel mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), pamoja na maendeleo katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

TRT World