Mamlaka za Uturuki hutumia neno 'kata makali' kuonesha namna magaidi walivyojisalimisha, kuuwawa au kukamatwa. / Picha: AA

Shirika la Kijasusi la Uturuki limefanikiwa kuwakata makali, kikundi kingine cha kigaidi cha PKK/KCK kaskazini mwa Iraq, vyanzo vya usalama vimeripoti.

Shirika la Kitaifa la Kijasusi la Uturuki (MIT) limemkamata Rojda Bilen, aliyepewa jina la Biseng Brusk, katika operesheni ya mpakani dhidi ya ugaidi, katika eneo la kijijini la Sulaymaniyah, nchini Iraq, vyanzo hivyo vimesema siku ya Jumanne.

Bilen alitambulika kama mratibu wa kikundi cha kigaidi huko Sulaymaniyah, viliongeza vyanzo hivyo, kwa sharti la kutotajwa jina kwa kuwa hawakuwa na ruhusa ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Alijiunga na kikundi hicho mwaka 2011 na alikuwa kwenye orodha ya magaidi wanaotafutwa "kwa kuwa mwananchama wa kikundi hicho," kiliongeza chanzo hicho.

Orodha hiyo imegawanywa kwenye vipengele vitano vya rangi, nyekundu ikiashiria wale wanaotafutwa sana, ikifuatiwa na bluu, rangi ya machungwa na rangi ya majivu.

Katika mapambano yake ya miaka 35 dhidi ya ugaidi nchini Uturuki, kikundi cha PKK, kimeorodheshwa kama kikundi cha kigaidi na serikali ya Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, kikiwa kimehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wanawake, watoto na watoto wachanga.

Kikundi cha kigaidi cha PKK hujificha kaskazini mwa Iraq, kikijiandaa kufanya mashambulizi dhidi ya Uturuki.

Mamlaka za Uturuki hutumia neno 'kata makali' kuonesha namna magaidi walivyojisalimisha, kuuwawa au kukamatwa.

TRT Afrika