Filamu iliyoshinda tuzo ya Holy Redemption itaendelea kusimulia hadithi ya Palestina / Picha: TRT World

Toleo jipya la TRT World, "Holy Redemption," limefanikiwa kuweka bayana ugaidi na ghasia za walowezi wa Israeli dhidi ya Wapalestina tangu kuonyeshwa kwake kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 24.

Filamu hii ya hali halisi iliyonyeshwa kwa wakati mmoja kwenye vituo sita vya kitaifa vya TRT wiki iliyopita na kushinda Tuzo ya Filamu na Programu Bora kwenye Tamasha la Kimataifa la Filamu Halisi la Al Jazeera, lililofanyika Sarajevo kuanzia Septemba 13-17.

Tamasha la 7 la Kimataifa la Filamu za Hali Halisi la Al Jazeera, moja ya matukio maarufu yanayokutanisha sekta ya filamu za hali halisi, lilijikita kwenye Palestina mwaka huu.

Kwa kaulimbiu "Haki?", tamasha hilo liliwaleta pamoja watengenezaji filamu za hali halisi, wasambazaji, wawakilishi wa vituo vya televisheni, na wataalamu wa vyombo vya habari kutoka duniani kote.

"Holy Redemption," ambayo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza kitaifa kwenye Sinema ya Atlas ya Istanbul mnamo Agosti 24, pia ilioneshwa kimataifa kwa mara ya kwanza kwenye tamasha hilo huko Sarajevo.

Kama moja ya filamu bora za tamasha hilo, ilishinda Tuzo ya Filamu na Programu Bora na ilipata sifa kubwa kutoka kwa watazamaji na wataalamu kutoka kote ulimwenguni.

'Holy Redemption' ilionyeshwa kwa mara ya kwanza kimataifa kwenye tamasha huko Sarajevo.

"Holy Redemption" inaleta kumbukumbu zenye uchungu za mauaji ya Srebrenica, yaliyotambuliwa kama mauaji ya kimbari na Umoja wa Mataifa, na inaonyesha mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israeli huko Palestina.

Kuonyeshwa kwa filamu hiyo nchini Bosnia, ambako kumbukumbu za Srebrenica bado ziko hai, kunaunda uhusiano wa kihisia kati ya mauaji haya mawili ya kimbari.

Tangu Oktoba 7, ambapo mauaji ya kimbari ya Gaza yalianza, TRT World imetoa filamu inayoangazia uhalifu wa pili wa kisiri unaotendeka.

"Holy Redemption" inaonyesha uporaji wa ardhi unaofanywa na walowezi wa Israeli kupitia macho ya mashahidi na wahusika wa uhalifu huo. Upigaji picha wa filamu hiyo ulianza miezi miwili baada ya Timu ya Uchunguzi ya TRT World kujipenyeza kwenye makundi ya Waisraeli wenye msimamo mkali katika Ukingo wa Magharibi, kufuatia kuanza kwa mauaji ya kimbari ya Gaza mnamo Oktoba 7.

Inatoa picha ya jinsi ardhi za Wapalestina zinavyokaliwa polepole kwa msaada wa Israeli. Kupitia picha zilizopatikana kutoka ndani ya vituo vya makazi ya kundi la msimamo mkali linalojulikana kama "Hilltop Youth"—linalotajwa na vyombo vya habari vya Israeli kama toleo la Israeli la wanamgambo wa ISIS—mchakato huo unafichuliwa kwa ulimwengu kwa mara ya kwanza.

Wahalifu na Mashahidi wa Uvamizi Wanazungumza Katika Filamu Hii

Mahojiano na wanaharakati wa Israeli, wanajeshi wa zamani wa Israeli, viongozi wa walowezi wenye msimamo mkali, na wanachama wa bunge la Israeli yanafichua mikakati ya Israeli ya kuwaondoa Wapalestina na kuiba ardhi kwa njia ya kimfumo.

Filamu hiyo inaonyesha jinsi makazi haramu yanavyozinduliwa na nyumba za Wapalestina zinavyoharibiwa.

Mahojiano muhimu kwenye filamu hiyo ni pamoja na Daniella Weiss, kiongozi wa walowezi; Zvi Sukkot, mwanachama wa zamani wa Vijana wa Vilima (Hilltop youth) na mbunge wa sasa; Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli Ehud Olmert; wakili mwanaharakati Michael Sfard; Hagit Ofran, kiongozi wa harakati ya Peace Now; na Nadav Weiman, mlinzi wa zamani wa kikosi maalum cha jeshi la Israeli.

"Holy Redemption" Iliyoshinda Tuzo Itaendelea Kusimulia Hadithi ya Palestina

"Holy Redemption," iliyoshinda Tuzo ya Filamu Bora na Programu Bora kwenye Tamasha la Kimataifa la Filamu za Hali Halisi la Al Jazeera, imepongezwa tangu kuonyehshwa kwake kwa mara ya kwanza kwa uwezo wake mkubwa wa kusimulia, ushahidi wa kuvutia, na ujasiri wa kufichua dhuluma katika eneo hilo.

Ikisifiwa kama ushindi wa uandishi wa habari wa uchunguzi, filamu hiyo imepongezwa na jopo la majaji na washiriki wa tamasha kwa ujumbe wake wenye athari kubwa na jukumu lake katika kutoa sauti ya kweli kuhusu mauaji ya kimbari ya Palestina.

Tuzo hii ina maana zaidi kwetu kuliko ile ya "Emmy" tuliyopokea hivi karibuni kwa sababu lengo letu ni kuhamasisha uelewa wa kimataifa kuhusu mauaji ya kimbari ya Palestina kupitia filamu yetu. /Picha: TRT World

Naibu Meneja Mkuu wa TRT Omer Faruk Tanrıverdi pia alihudhuria maonyesho maalum ya filamu hiyo. Baada ya kuonyeshwa kwa filamu hiyo, Tanrıverdi alisema:

“Kwa kuonyeshwa kwa filamu yetu huko Sarajevo, tumesisitiza kuwa mauaji mengine ya kimbari yanatokea mbele ya macho ya dunia kwenye ardhi hizi ambapo majeraha ya Srebrenica bado kupoa. Ndani ya dakika 53, tumeanika sera za miaka 75 za uvamizi wa Israeli na tumeonyesha kwa uwazi ukatili wa walowezi wenye msimamo mkali wa Israeli huko Palestina. Tuzo hii ina maana zaidi kwetu kuliko ile ya "Emmy" tuliyopokea hivi karibuni kwa sababu lengo letu ni kuhamasisha uelewa wa kimataifa kuhusu mauaji ya kimbari ya Palestina kupitia filamu yetu. Kama TRT World, tumekuwa tukiiunga mkono mapambano ya Wapalestina hata kabla ya Oktoba 7, na 'Holy Redemption' ni matokeo ya juhudi hizo. Tunatumaini kila mtu atatazama na kushiriki mafanikio haya makubwa ya uandishi wa habari.”

Katika siku zijazo, "Holy Redemption" itaendelea kuonyeshwa kwenye majukwaa mbalimbali ya kimataifa, ikiweka mwangaza wa kimataifa juu ya mauaji ya kimbari ya Palestina.

Tazama Filamu hiyo:

TRT Afrika