Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonya kuwa demokrasia ulimwenguni iko mashakani.
Akizungumzia hali ya kisiasa barani Ulaya, Erdogan aligusia ongezeko la “miunguwatu kama ilivyojidhihirisha kwenye chaguzi za hivi karibuni.”
Kauli yake inakuja huku kukiwa na hofu ya ongezeko la vuguvugu dhidi ya wahamiaji barani Ulaya.
Uturuki, suluhisho pekee kwa Umoja wa Ulaya
Erdogan alisisitiza kuwa Umoja wa Ulaya unapitia changamoto kadhaa zikiwemo za kiuchumi, kiulinzi, na kisiasa.
“Ni Uturuki tu itakayoweza kuisaidia Umoja wa Ulaya,” alisisitiza Erdogan, akigusia umuhimu wa kimkakati wa Uturuki kwa utulivu wa Ulaya na ushawishi ulimwenguni.
Kushindwa kwa mataifa ya magharibi huko Gaza
Akizungumzia hali ya kibinadamu huko Gaza, Erdogan alikashifu taasisi za magharibi kushindwa kuchukua hatua.
“Taasisi za magharibi na viongozi wao wamekaa kimya huku watu zaidi ya 61,000, wengi wakiwa ni wanawake na watoto wakiuwawa kinyama,” alisema.
Kauli yake Erdogan inaashiria nafasi ya Uturuki katika siasa za ulimwenguni.