Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kufikiwa kwa taifa huru la Palestina, na linalotambulika kijiografia kwa msingi wa mipaka ya 1967, na Jerusalem kama mji mkuu, hakuwezi kucheleweshwa tena.
"Amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati inawezekana tu kupitia suluhu la mwisho la mzozo wa Palestina na Israel," Erdogan alisema Jumapili katika sherehe za ufunguzi wa Kanisa la Orthodoksi la Mor Efrem Syriac huko Yesilkoy upande wa Ulaya wa Istanbul.
Erdogan alisema uturuki iko tayari kufanya sehemu yake kusimamisha mzozo wa Israel na Palestina, na kupunguza mvutano ulioongezeka siku ya Jumamosi.
Kundi la Wapalestina la Hamas lilianzisha Operesheni ya Mafuriko ya Al Aqsa, likisema ni kujibu mashambulizi ya Msikiti wa Al Aqsa na kuongezeka kwa ghasia za walowezi. Ilisema ilirusha makombora na kuwakamata Waisraeli wengi.
Katika kulipiza kisasi, jeshi la Israel lilianzisha Operesheni ya Upanga wa Chuma dhidi ya Hamas, na kuanzisha mashambulizi ya anga kwenye mji wa Gaza.
Mapigano yaliendelea hadi siku yake ya pili Jumapili na Israeli ilitangaza "hali ya vita".