Heritier Luvumbu. Picha Rayon Sports 

Mshambulizi wa DR Congo Heritier Luvumbu alikuwa amesalia na miezi mitano kukamilisha mkataba wake ambao ungeisha Juni 30 hata hivyo, mechi yake dhidi ya Polisi imekuwa ndio yake ya mwisho akiiwakilisha Rayon Sports FC.

Haya yote yalianza kwenye mechi ya ligi kuu ya soka nchini Rwanda (RPL) klabu ya Rayon FC ilipokuwa ikichuana na Polisi FC, Luvumbu akisherehekea bao lake kutumia ishara ya kuziba mdomo wake, akielekeza vidole vyake viwili kwenye kichwa chake.

Kufuatia ishara hiyo, shirikisho la soka la Rwanda FERWAFA lilimsimamisha kusakata soka na kushiriki shughuli zinazohusiana nazo nchini humo kwa miezi sita.

Rayon Sports ilijitenga na ishara ya Luvumbu na kuiita "mwenendo mbaya" kabla ya kutangaza kujitenga naye mara moja.

Baada ya tukio hilo, Héritier Luvumbu amerejea DRC na kupokewa na rais mratibu wa Klabu ya As Vita Amadou Diaby na kuonesha mshikamano kwa Héritier Luvumbu ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo.

TRT Afrika na mashirika ya habari