Mfululizo wa Ikechukwu Nnadi unaonyesha uhusiano thabiti kati ya akina mama na binti. Picha: Ikechukwu Nnadi

na

Pauline Odhiambo

Ikiwa maneno hayatoshi kuelezea upendo kati ya mama na binti, basi labda mchoro unaweza kuelezea vizuri zaidi uhusiano wao imara. Hiyo ndiyo imani ya msanii wa Nigeria, Ikechukwu Nnadi.

Baada ya kuzaliwa kwa binti yake, Nnadi alivutiwa sana na uhusiano huu wa mama na binti kiasi cha kuanza kuchora kazi zinazohusu uhusiano huo wa kipekee.

“Kusikia habari kwamba mke wangu atajifungua msichana kulibadilisha maisha yangu. Ilinisukuma kufikiria kwa kina kuhusu mahusiano kati ya mama na binti, na kuyaelezea hayo katika sanaa yangu,” Nnadi anaiambia TRT Afrika.

Picha Kamili

Michoro wa Nnadi ulibadilika kutoka kwa uhalisia kupita kiasi hadi mtindo halisi wa uchoraji. Picha: Ikechukwu Nnadi

Lakini kurekodi hisia kila mara kumejumuishwa sanaa ya Nnadi. Jaribio lake la kwanza katika picha lilikuwa limechochewa na baba yake – mpiga picha mwenye jicho kali na ya kipekee.

“Nilipokuwa mvulana, nilikuwa na azma ya kuchora picha kamili ya baba yangu, hivyo niliendelea kuchora kuendana na sura yake,” msanii huyo mwenye umri wa miaka 34 anakumbuka.

“Nilichora picha ile ile tena na tena mpaka hatimaye nilipata sifa zake zote sawa.”

Mapenzi yake ya ukamilifu hatimaye yalimpeleka Nnadi kwenye sanaa ya hali halisi kabisa – ujuzi ambao aliuimarisha wakati wa masomo yake ya sekondari na chuo kikuu.

“Nilipata oda yangu ya kwanza kutoka kwa rafiki wa dada yangu nilipokuwa bado niko shule ya sekondari. Kulipwa kwa kitu ninachokipenda kufanya kulikuwa na motisha kwa sababu kulinisaidia kujitunza mwenyewe nilipofika chuo kikuu,” anasema.

Msanii Halisia

Hali ya kihisia inayotambulika ya wahusika hufanya picha za kuchora zihusiane na mtazamaji. Picha: Nnadi

Mtindo wake umeendelea kubadilika kwa muda, ukibadilika kutoka hali halisi kabisa hadi mtindo wake wa sasa. “Ilitumia miaka mingi na mazoezi kukuza uchoraji wangu,” anasema msomi huyo wa sanaa.

“Hata ninapokuwa ninamchora mtu, kwanza nawaruhusu kupumzika na kupotelea mawazoni mwao ili niweze kurekodi na kuelewa hali yao ya kiakili vizuri zaidi,” Nnadi anaelezea.

“Najaribu kufikiria jinsi ninavyotaka waonekane katika michoro na kulinganisha hilo na hadithi zilizo moyoni mwangu. Hii ni kitu ninachotaka watu waone wanapotazama sanaa na michoro yangu.”

‘Portrait of a Lady’ ni mfululizo unaoonyesha wanawake katika hali tofauti za kutafakari. Picha: Nnadi

Gharama ya karatasi

Kazi zingine za Nnadi, ni ‘Picha ya Mwanamke’ au "Portrait of a lady" ambayo inaonyesha wanawake mbalimbali katika mazingira tofauti za fikra.

Pia amefanya kazi zake binafsi na kazi nyingine inayoitwa Anwulika ambao maana yake ni ‘furaha yangu ni kubwa’ katika lugha ya Igbo.

Furaha ya Nnadi ya kuchora labda inapunguzwa tu na bei ya baadhi ya vifaa vyake.

"Anwulika" unamaanisha ‘furaha yangu ni kubwa zaidi’ katika lugha ya Kiigbo. Picha: Nnadi

“Inakuwa vigumu kupata karatasi yenye ubora unaofaa hivyo inabidi niagize karatasi zote ninazohitaji, na hilo linaweza kuwa ghali,” anasema.

“Karatasi ya pasteli ninayotumia inaagizwa kutoka nje, na hilo linaongeza sana gharama ya vifaa vya uchoraji.”

Mara nyingi Nnadi analazimika kuagiza aina fulani za turubai pia.

Amini safari yako

“Nina matumaini kwamba siku moja makampuni yanayotengeneza vifaa hivi vya sanaa yatafungua maduka yao Nigeria ambayo nadhani itasaidia kupunguza gharama,” anatafakari. “Labda pia wanapaswa kufikiria kuwafanya wasanii wa ndani kuwa mabalozi wao ili wasanii waweze kupata vifaa wanavyohitajika kwa bei nafuu.”

Sanaa ya Nnadi imeonyeshwa katika majumba ya sanaa nchini Nigeria na Ufaransa. Picha: Nnadi

Michoro mingi ya Nnadi imewekwa katika nyumba za sanaa na monesho nchini Nigeria na Ufaransa.

Ushauri wa Nnadi kwa wasanii wanaochipukia: “Amini safari yako ya sanaa na uendelee nao. Jipe nafasi ya kufanya makosa. Makosa hayo yatakusaidia kuumbika kuwa msanii unayekusudiwa kuwa.”

TRT Afrika