Chukwu, mchoraji aliyepata umashuhuri kupitia kazi ya kuchora mbele ya kadamnasi / Picha: Isaac Chukwu

Na

Pauline Odhiambo

Uchoraji mbele ya hadhira ni ujuzi ambao Isaac Chukwu aliyoubobea na kujitengenezea nafasi muhimu katika ulimwengu wa sanaa kwa kuwachora wahusika wake 'kichwa chini miguu juu'.

Uchoraji wake mbele ya kadamnasi , unaojulikana pia kama uchoraji wa uigizaji, kwa hakika umeinua usanii wa Chukwu - ameachana na mtindo wa zamani na kuanza kuchora katika muda mfupi katika shughuli mbalimbali za usanii nchini Ghana.

"Njia ya juu chini kimsingi ni kuchora tu kwa mfumo wa kinyume, naanza kwa kuchora maeneo ya tumbo kisha polepole nahamia kichwa," msanii huyo wa Ghana-Nigeria anaiambia TRT Afrika.

"Muda mfupi zaidi ambao nimechukua kukamilisha picha kama hii ni kama dakika 2. Ni wakati ule ule niliomchora (rapa wa Ghana) katika jalada la albamu ya Sarkodie wakati wa tamasha mnamo 2018.

Mchoro huo ulinunuliwa muda mfupi baadaye na mwigizaji wa Hollywood Idris Elba ambaye alikuwa amehudhuria tamasha katika mji mkuu Accra.

Tangu wakati huo Chukwu amewachora wanamuziki kadhaa wa Afrika Magharibi akiwemo Shatta Wale, Stonebwoy na mtayarishaji wa muziki kutoka Nigeria Don Jazzy miongoni mwa nyota wengine.

Aliwahi kuchora hadi picha tisa kwa mfumo wa kinyume nyume katika sherehe ya kutolewa kwa tuzo - picha hizo ziliwasilishwa kwa washindi wote waliotajwa kwenye hafla hiyo.

"Pia nimemchora Makamu wa Rais (Mahamadu Bawumia) katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika kwa heshima yake. Picha yake ilikuwa tayari kuonyeshwa mwishoni mwa chakula,” asema.

Nilipenda kuchora toka nikiwa mtoto

Chukwu anashukuru ujuzi wake wa uchoraji wa juu chini kwa kutazama mara kwa mara wachoraji wengine kwenye kipindi maarufu cha talanta kinachotangazwa kote duniani katika nchi nyingi. Pia alichukua vidokezo zaidi juu ya ustadi huo kwa kumtazama mchoraji mwenzake wa Ghana akifanya kazi.

Chukwu mwenye umri wa miaka 26 amechora hadi picha 300 za kitaalamu kulingana na makadirio yake, nyingi zikiwa ni picha za watu muhimu wanaosherehekea siku za kuzaliwa na karamu za ukumbusho, hapo ndipo wanapotoka wateja wake.

Sherehe zinapoendelea, Chukwu - ambaye kipachiko cha kutundukia michoro yake mara nyingi huwekwa katikati mwa jukwaa au upande ambapo watazamaji wanaweza kutazama michoro yake kwa njia ya moja kwa moja - akichora kwa urahisi. Kujiamini huku akicheza kwake na brashi ni dalili tosha kuwa ana uzoefu wa muda mrefu.

"Sijawahi kuwa mwanafunzi mwerevu zaidi lakini wanafunzi wenzangu mara nyingi waliniomba nichore kwenye madaftari zao baadhi ya michoro katika masomo ya sayansi," anakumbuka.

Mwigizaji wa Hollywood Idris Elba alinunua mchoro wa Chukwu mwaka wa 2018. Picha: Isaac Chukwu

"Wakati huo, nilifikiri ni jambo nililopenda kulifanya utotoni. Haikuwa jambo nililolichukulia kwa uzito.”

Mamake Chukwu, mwalimu katika shule yake, alimhimiza kuweka bidii zaidi katika masomo yake lakini Chukwe alipenda kucheza mpira wa kikapu au mpira wa miguu na kufanya shughuli nyingine.

Mpaka pale baba yake alipopata dharura ya matibabu mnamo 2012, ndio hatimaye Chukwa alianza kuichukulia sanaa yake kwa uzito.

"Baba yangu alipatwa na kiharusi na hiyo ndiyo ilikuwa imeniamsha kutoka usingizini kwa sabab kama mtoto wa kwanza, ilibidi nichukue jukumu la kumtunza mama yangu na ndugu zangu watatu."

Uanagenzi

Kuwa skauti na mpiga ngoma katika kikundi cha muziki wa matembezi shuleni kulimfanya afikirie kujiunga na jeshi baada ya shule ya upili lakini hali ngumu ya mafunzo ya kijeshi ilimfanya aachane na wazo hilo haraka.

Chaguo lake lililofuata lilikuwa kucheza michezo katika kiwango cha taaluma, lakini kwa kuhimzwa na walimu wake wa sanaa, Chukwu aliamua kuipa sanaa kipao mbeli.

"Niliweka bidii yangu yote katika sanaa na nilifanya kazi kama mwanagenzi kwa muda mrefu baada ya shule ya upili kabla ya kusomea sanaa ya kibiashara," asema. "Kwa kweli nilianza kuchora hadharani kanisani kama njia ya kuwaheshimu wachungaji wanaonitembelea. Mara nyingi nililinganisha kasi yangu ya uchoraji na kipindi cha kwaya ili kufikia wakati walipokuwa wamemaliza kuimba, uchoraji uwe tayari kwa kuonyeshwa.”

Chukwu alikuza biashara yake ya sanaa pole pole kwa usaidizi wa wateja wanaohudhuria na walioanza kumkaribia ili kuwatumbuiza katika siku za kuzaliwa na maadhimisho ya mwaka.

"Kanisa lilikuwa eneo langu la faraja kwa sababu mara nyingi nilipewa muda zaidi wa kukamilisha michoro baada ya mahubiri," asema Chukwu ambaye amekuwa mtaalamu wa uchoraji kwa miaka minane.

"Kuchora kwenye hafla zingine kulinisaidia kuboresha ustadi wangu na kunifanya nijifunze jinsi ya kuinua utendakazi wangu kupitia michoro ya mkato wa herufi."

Ukataji wa herufi ni aina ya uchoraji wa maneno, nukuu au herufi za kwanza ambazo ni za kutia moyo. Chukwu hutega vikato hivi kwenye turubai kisha kuipaka rangi ili kukamilisha mchoro.

"Baadhi ya wakati mimi hukata herufi kwenye studio na kujirekodi nikichora ili mteja aonyeshe mchakato mzima kwenye hafla yao," anasema mpiga picha wa video na mtayarishaji wa maudhui, ambaye wakati mwingine hubadilishana vikato vya herufi kwa nambari au vipande vya picha vya kufungamana.

"Sehemu nyingi za video ninazochapisha kwenye mitandao yangu ya kijamii kwa kweli hurekodiwa kwa kutumia kamera ya simu yangu."

Uchoraji wa bila kuangalia

Chukwu pia anafanya kazi kama meneja wa uzalishaji katika jumba la sanaa huko Accra - kazi ambayo ameifanya kwa miaka minne na ambayo anathamini kiwango chake cha ustadi kinachokua.

"Kusakinisha na kuonyesha kazi za sanaa za wasanii tofauti kote barani Afrika kumeunda jinsi ninavyoona sanaa yangu mwenyewe, na hiyo kwa kiasi fulani imeathiri mchakato wangu wa kuunda maudhui, anasema."

Alianza uchoraji akiwa amefumbwa macho katika maonyesho yake hadharani lakini anasema ni ujuzi ambao bado anahitaji muda kuukamilisha.

Chukwu pia hufurahia ushirikiano na washairi, mpiga saksafoni na wasanii wengine - kuoonyesha sanaa zao na maonyesho ya utendaji wao,

"Kwa sasa ninafanya kazi na mzingaombwe ili kuona ni aina gani ya onyesho tunaloweza kuwaonyesha watazamaji wanaothamini sanaa na mazingaombwe," anaiambia TRT Afrika. "Siku zote ni nzuri kuona jinsi watazamaji tofauti wanavyoitikia sanaa katika aina zake tofauti."

TRT Afrika