Msanii  Patoranking ahitimu Chuo Kikuu cha  Harvard

Msanii  Patoranking ahitimu Chuo Kikuu cha  Harvard

Wasanii mbalimbali nchini Nigeria wameungana kumpongeza Patoranking .
Msanii Patoranking alijizoelea umaarufu kupitia wimbo wake wa 2013 wa Alubarika. Picha: Patoranking/ Instagram

Msanii wa Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie, ambaye anajulikana na wengi kama Patoranking, amehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Havard.

Msanii huyo anayevuma na wimbo wa “My Woman, My Everything” alitoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumapili.

"Karibuni kwenye ulimwengu mpya wa @harvardhbs Alumnus,” aliandika katika ukurusa huo.

Wasanii wa Nigeria waliungana kumpongeza Patoranking kufuatia mafanikio hayo.

Patoranking amejizoelea umaarufu siku za karibuni baada ya taasisi yake kushirikiana na ALX Africa, kusaidia wanafunzi katika masuala ya mitandao.

Patoranking amepongezwa na watu mbalimbali kufuatia hatua hiyo./Picha: 

"Tumejiwekea lengo la kuandaa Waafrika milioni 1 ndani ya miaka 10 ijayo. Tunaamini katika wingi wa vipaji vya kipekee na waleta mabadiliko barani Afrika na tutaendelea kupinga ukosefu wa usawa wa kifedha unaozuia kuibuka kwao,’’ Patoranking alisema katika uzinduzi huo.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 33 alijipatia umaarufu 2013 baada ya kutoka kwa wimbo wake wa Alubarika.

Nyimbo za Patoranking za "Daniella Whine" na "My Woman, My Everything" zimeorodheshwa kwenye chati ya nyimbo kumi bora za MTV Base.

Ameshinda tuzo nyingi, zikiwemo Tuzo za Sound City Viewers Choice na Tuzo za Video Bora kwa wimbo wake wa ‘Heal the World’.

TRT Afrika