Wasimamizi wa tuzo za AFRIMA wamesisitiza umuhimu wa kudhibiti na kuimarisha usimamizi wa tasnia ya burudani ya muziki huku ikiungana na mamilioni ya vijana wa Kiafrika na mashabiki wa muziki kumuomboleza mwanamuziki wa Nigeria Mohbad.
Rais wa AFRIMA, Mike Dada, ameeleza kupitia taarifa yake kuwa, uanzilishi wa tasnia ya muziki/burudani unastahili kupewa kipaumbele cha juu ili kukabiliana na mazoea yasiyo ya kitaalam ambayo yamedumu muda mrefu kwenye sekta hiyo ya mziki Barani Afrika.
Dada ametaja kuhuzunishwa na kifo cha Mohbad na kuongeza kuwa Afrika imepoteza talanta ya ukweli katika tasnia yake ya muziki inayokua kwa njia ya kushangaza,
Mwimbaji wa Nigeria, Mohbad, (majina halisi Ileri Oluwa Oladimeji Aloba) alifariki katika hali ya kushangaza siku ya Jumanne, Septemba 12, 2023, huku mauaji yake yakiendelea kuchunguzwa na polisi.
Nyota huyo chipukizi wa muziki mwenye umri wa miaka 27 anayejulikana pia kama Imole (Mwanga) alikuwa msanii mchanga na mustakbali nzuri ambaye amekua kwa haraka kutokana na ubunifu wake na kipaji chake cha kushangaza huku akitoa maneno ya kusisimua sana yaliyogusa mioyo ya mamilioni ya mashabiki kote ulimwenguni.
Kwa niaba ya kamati YA Kimataifa ya Tuzo za AFRIMA, tunaomboleza na Sekta ya Muziki ya Nigeria, wazazi na mashabiki wa Mohbad, juu ya kifo chake chenye uchungu. Kifo Cha Mohbad ni tukio la kusikitisha ambalo limetuacha sote na huzuni kubwa. Mawazo na sala zetu zote ziko pamoja na familia na wapendwa wa marehemu katika wakati huu mgumu.
"Kupitia kifo chake, Afrika imepoteza talanta yenye mustakbali bora katika tasnia yetu ya muziki na burudani inayokua. Tunamwomba Mola ampe pumziko la milele, na awape wazazi wake, familia na mashabiki ujasiri wa kuhimili uchungu wa kifo hicho kisichoweza,” Dada alisema.
"AFRIMA inaongoza juhudi za kuhamasisha wadau katika tasnia ya ubunifu Barani Afrika, kwa kuzingatia Nigeria, ili kuanzisha shughuli za kitaasisi na kudhibiti tasnia ya burudani ya muziki,” Dada alimaliza.
"Ni muhimu kuwa na sheria ambayo inasimamia sekta ya muziki ili kuzuia kuwa 'huru-kwa-wote,' kama ilivyo kwa sasa, kwani mahitaji ya kuingia ni ya chini mno hadi mtu yeyote anaweza tu kuamka na kuanzisha studio ya rekodi ya muziki."
AFRIMA inasema kuwa itatumia jukwaa lake ili kuandaa mkutano wa wadau ikiwa na nia ya kushirikisha mkono wa sheria wa serikali kote Afrika kupitia Umoja wa Afrika.