Iwaju: Watengenezaji filamu wanaipa Afrofuturism utambulisho mpya

Iwaju: Watengenezaji filamu wanaipa Afrofuturism utambulisho mpya

Afrofuturism inapata umaarufu zaidi na kiu kutokana na mitazamo mipya kuhusu hadithi za Kiafrika
Iwaju ilitayarishwa na Disney kwa ushirikiano na Kugali. Picha: Disney

Na Charles Mgbolu

Vijana watatu wa Kiafrika wamepata sifa kimataifa kwa majukumu yao katika tamthilia mpya ambao sasa unaoneshwa kupitia kamouni la Kimarekani la video la Disney Studios.

Toluwalakin Olowofoyeku, Olufikayo Ziki Adeola, na Hamid Ibrahim, marafiki watatu kutoka Nigeria na Uganda, wametengeneza Kugali, kampuni ya burudani ya Kiafrika ambayo Disney imeanzisha ushirikiano nayo.

Watatu hao walifanya kazi kutengeneza tamthilia ya katuni yenye sehemu sita uitwao Iwaju, ambao unasimulia majadiliano ya msichana mdogo anayejitahidi kufichua bosi wa genge la utekaji nyara mjini Lagos nchini Nigeria.

Mandhari za afrofuturism zinazoonekana katika matukio zinaonyesha mji wenye shughuli nyingi wa Nigeria katika mwanga mpya, na magari yanayoruka yakipita ndani na nje ya majengo ya kikompyuta, na roboti kama wanyama.

Adeola, ambaye aliandika skripti, anasema kuweka hadithi za Kiafrika katika ulimwengu wa AI bila shaka ni mustakabali kwa uwasilishaji hadithi za Kiafrika.

Iwaju ilitayarishwa na Disney kwa ushirikiano na Kugali. Picha: Disney

‘’Dunia ikitazama ukuaji wa haraka wa akili mnameba, tunahitaji watengenezaji filamu na waigizaji kuikumbatia uasilia wetu, ambao unatufanya tuwe wa pekee na tofauti kama Waafrika. Hicho ndicho kitakachofanya dunia itutambue katika utaratibu mpya wa dunia wa teknolojia,’’ Adeola anaiambia TRT Afrika.

Afrofuturism inapata uhai mpya na kiu ya mitazamo mipya kuhusu hadithi za Kiafrika. Mafanikio ya filamu kubwa za Hollywood kama Black Panther yamezidi kuipa umaarufu mandhari hii.

Adeola, akiwa na marafiki zake wa utotoni Tolu Olowofoyeku na Hamid Ibrahim, wanasema lengo lao ni kuunda jukwaa linalotoa mamilioni ya mashabiki na hadithi zilizoongozwa na utamaduni wa Kiafrika kwa kutumia sanaa, uhalisia, na ukweli ulioongezewa ubunifu.

‘’Jambo muhimu ni kuongeza ubora. Wakati uasilia unapokutana na uwasilishaji hadithi wa ubora wa juu, mambo ya kimiujiza yanatokea, na nadhani ni mwanzo wa kitu kizuri kwa uhuishaji na utengenezaji katuni Afrika,’’ anaongeza.

Ubora ni muhimu, kwani watengenezaji filamu vijana walilazimika kufanya kazi na mada ya hadithi isiyo ya kawaida: afrofuturism, ambayo ni aina ya kitamaduni inayochanganya sayansi, historia, na hadithi ili kueleza uzoefu wa Kiafrika.

Adeola (kushoto) alifanya kazi na Tolu Olowofoyeku na Hamid Ibrahim. Picha: Kugali

Wataalam wanasema ililenga kuunganisha wale kutoka diaspora nyeusi na asili yao ya Kiafrika iliyosahaulika.

Adeola anasema ilikuwa muhimu kuzungusha sifa hii ya Afrofuturistic ili kuongezea upekee wa mtoto wa Kiafrika, ambaye anaonyeshwa katika tamthilia kama msichana wa miaka 10, mwenye akili.

‘’Uwasilishaji wa wahusika wa Kiafrika katika vyombo vya habari mara nyingi huchunguzwa na wasio Waafrika au kuzingatia mada hasi. Moja ya mambo mazuri tuliyonayo kuhusu wahusika ni ubunifu wao na ujanja.

‘’Nilitaka kuonyesha kwamba kipaji hakina kikomo kwa mazingira yako ya kijamii-kiuchumi, nadhani watu wataangalia hili na kutambua kwamba tuna ubunifu wetu, tunapamba tamaduni yetu, na tuna mambo yetu wenyewe.’’

Waziri wa Utamaduni wa Nigeria, Hannatu Musawa, alisifu onyesho hilo katika uzinduzi wake Lagos, akisema: "Hii ni kubwa kwa Nigeria kwa sababu hatimaye sasa tuna hadithi zetu wenyewe zikisimuliwa kutoka mtazamo wetu wenyewe."

Mfululizo wa sehemu sita unajumuisha Pidgin ya Nigeria, mchanganyiko wa Kiingereza na lugha za kienyeji, na wahusika wote wanapewa sauti na waigizaji kutoka nchi ya Afrika Magharibi.

TRT Afrika