Mamlaka za Afrika Kusini zinasema kuwa chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana.
Hata hivyo, Waziri anayehusika na Jeshi la Polisi nchini humo, Senzo Mchunu, alisisitiza kuwa mamlaka za uchunguzi kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Pretoria, bado zilikuwa zinaendelea na uchunguzi.
“Tuna imani kubwa kubwa na timu zetu za uchunguzi. Ni vyema wale waliotekeleza tukio hilo wajisalimishe wenyewe au tuwatafute wenyewe,” alisema Mchunu.
Mauaji hayo yalitokea siku ya Ijumaa jioni katika mji wa Lusikisiki, ulioko Jimbo la Mashariki.
Picha za video kutoka polisi
Picha za video za polisi zilionesha tukio hilo likitokea katika nyumba mbili zilizo katika eneo moja, nje kidogo ya jiji hilo.
Wanawake12 na mwanaume mmoja waliuwawa ndani ya nyumba moja, wakati wengine watatu na mwanaume mmoja waliuwawa katika nyumba nyingine, jeshi la polisi limesema.
Wanawake watatu, mwanaume mmoja na mtoto mchanga walisalimika katika tukio hilo.
Kulingana na vyombo vya habari katika eneo hilo, watu hao walikuwa wanahudhuria shughuli ya kifamilia wakati tukio hilo linatokea, japo sababu ya mauaji hayo bado haijajulikana.
Afrika Kusini, yenye idadi ya watu milioni 62, imeshuhudia mauaji 12,734 ndani ya miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2024, kulingana na takwimu kutoka idara ya makosa ya kiuhalifu ya jeshi la polisi nchini humo.