Wananchi nchini Mali waliidhinisha kwa wingi mabadiliko ya katiba katika kura ya maoni, kuashiria hatua muhimu katika mipango ya kurejesha utawala wa kiraia.
Hii ni kulingana na matokeo ya muda yalivyoonesha Ijumaa.
Uongozi wa kijeshi umeifanya rasimu ya katiba kuwa msingi muhimu wa kuijenga upya Mali.
Asilimia tisini na saba ya kura za maoni zilipigwa kuunga mkono mabadiliko hayo, halmashauri ya kusimamia uchaguzi ilisema. Idadi ya wapiga kura ilikuwa asili mia 39.4 ya waliojisajili.
Rais mwenye nguvu
Katiba mpya itaimarisha nafasi ya rais, mabadiliko ambayo yamezua matarajio kuwa kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita ananuia kuwania nafasi hiyo.
Mabadiliko hayo pia yatatoa fahari ya nafasi kwa vikosi vya jeshi na kusisitiza "umuhimu wa taifa huru'' ajenda waliotangaza tangu jeshi ilipoingia madarakani mnamo 2020.
Upigaji kura ulitatizwa katika miji mingi katikati na kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi , ikiwa wananchi wengine walikuwa na hofu ya mashambulizi au kutoelewana kisiasa.
Wapinzani wa mpango huo wanaona kura hiyo kama iliyokusudiwa kuwaweka viongozi katika jeshi madarakani zaidi ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Februari 2024, licha ya dhamira yao ya awali ya kukabidhi kwa raia baada ya uchaguzi.