Mkakati wa 2024-2028  unalenga kusukuma mbele nafasi ya Uturuki katika uwekezaji wa kimataifa wa moja kwa moja kwa asilimia 1.5, amesema Burak Daglioglu / Picha: AA

Ofisi ya Rais wa Uturuki ya Uwekezaji imewasilisha "Mkakati wa Uturuki wa Uwekezaji wa Moja kwa Moja: 2024-2028" kwa wawekezaji wa dunia katika Mkutano wa mwaka 2024 ujulikanao kama Brand Finance Global Soft Power mjini London.

Uchumi imara wa Uturuki na mfumo himilivu unaiweka nchi kama sehemu sahihi ya wawekezaji wa kimataifa, Mkuu wa Ofisi ya Uwekezaji Burak Daglioglu, amesema, katika mkutano siku ya Jumatano.

Amesisitiza jukumu la Uturuki kama nchi inayoongoza kwa uwekezaji katika eneo, akionyesha uchumi wake imara katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Daglioglu pia ameongelea umuhimu wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kimataifa katika kukuza mazingira bora ya uwekezaji na kuonyesha mabadiliko ya kimfumo yaliyofanyika katika Ofisi ya Rais ya Uwekezaji ili kurahisisha mchakato wa uwekezaji nchini Uturuki.

"Kama Ofisi ya Rais ya Uwekezaji, tumedhamiria kushambaza fursa nyingi za Uturuki kwa wawekezaji wa dunia. Leo, hapa London, tulipata fursa ya kuwashirikisha wadau muhimu, kupaza sauti ya jitihada zetu za diplomasia ya uwekezaji," amesema.

Ukuaji imara wa uchumi

Akitilia msisitizo wa mafanikio ya Uturuki katika kuvutia uwekezaji, Daglioglu amebaini kuwa zaidi ya kampuni 700 za kimataifa zinafanya kazi katika vituo vya teknoloji na R&D, huku zaidi ya kampuni 80,000 za kimataifa zikitoa huduma mbalimbali katika sekta tofauti.

Kuongezeka kwa uwekezaji wa kimataifa Uturuki katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili kumepita kiwango cha kuridhisha cha bilioni $260, amesisitiza.

Kuangalia mbele, Daglioglu ameweka bayana mpango unaokuja wa “Mkakati wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Moja kwa Moja: 2024-2028,” wenye lengo la kusukuma mbele nafasi ya Uturuki duniani katika soko la kimataifa la uwekezaji na kufikia asilimia 1.5, ikiwa ni hatua muhimu kutoka ile ya sasa ya asilimia 1.

Katika hotuba yake, Daglioglu amehimiza ukuaji imara wa uchumi wa Uturuki katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili, akisisitiza umuhimu wa nafasi yake katika uwekezaji wa kimataifa katika eneo hilo.

Msisitizo ukiwa ni katika kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa kigeni, amefafanua hatua za Ofisi ya Rais ya Uwekezaji, na mabadiliko yaliyofanyika yenye lengo la kuwezesha uwekezaji wa kimataifa nchini Uturuki.

TRT World