Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wawekezaji wake wa China wamefikia makubaliano juu ya ubia wao wa pamoja wa Sicomines wa shaba na cobalt, walisema katika taarifa siku ya Jumamosi, huku Wachina wakiwekeza hadi dola bilioni 7 katika miradi ya miundombinu.
Pande zote mbili zilikubaliana kudumisha muundo wa sasa wa umiliki wa hisa, wakati washirika wa China, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Sinohydro na China Railway, watalipa 1.2% ya mrabaha kila mwaka kwa Kongo, taarifa hiyo ilisema.
Kongo ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa cobalt, sehemu muhimu katika betri za magari ya umeme na simu za rununu.
Pia ni mzalishaji wa tatu kwa ukubwa wa shaba duniani na ina akiba kubwa ya lithiamu, bati, tungsten, tantalum na dhahabu.
Sekta ya madini ya Kongo, hasa migodi yake ya shaba na kobalti, sasa inatawaliwa na makampuni ya China.