Wasanii maarufu wa Afrobeats wa Nigeria wamehodhi orodha ya walioteuliwa katika vipengele vyote vya Afrika vya tuzo za Grammy 2024, huku Burna Boy akiongoza kundi hilo kwa kuteuliwa mara nne.
Mwimbaji Davido aliteuliwa mara tatu kwa tuzo za Grammy 2024 - ikiashiria kurejea kwake kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya walioteuliwa kwa zaidi ya miaka kumi.
Alichapisha kwenye X, ambayo zamani ilikuwa Twitter, kuhusu subira yake ya muda mrefu ya kurejea kwenye orodha: "Wateule 3 kwenye Grammys! Kuchelewa sio kukataliwa!"
Davido ameteuliwa kuwania kipengele cha 'Utendaji Bora Afrika' kwa wimbo wake wa 'Unavailable' aliomshirikisha Musa Keys.
Kuteuliwa kwa Tyla
Pia alipata uteuzi wa kitengo cha Utendaji Bora wa Muziki wa Ulimwenguni kwa wimbo wake 'Feel', huku albamu yake ya "Timeless" ikimpa uteuzi wa tatu katika kitengo cha Albamu Bora ya Kimataifa.
Mwimbaji wa Afrika Kusini Tyla alipata uteuzi wake wa kwanza katika kitengo cha kwanza cha Muziki wa Kiafrika cha Grammys kwa wimbo wake wa 'Water'.
Wasanii mahiri wa muziki wa Nigeria Davido, Burna Boy, Asake, Olamide, na Ayra Starr wote wamepata uteuzi katika kitengo hicho pia.
Burna Boy, hata hivyo, ndiye aliyeteuliwa zaidi, akitajwa mara nne katika kitengo cha utendaji bora wa muziki wa Kiafrika, kitengo cha Utendaji Bora wa Muziki Ulimwenguni, kitengo cha Albamu Bora ya Ulimwenguni na kitengo cha Utendaji Bora wa Melodic Rap.
Jina la kwanza Nigeria
Anakuwa msanii wa kwanza wa Nigeria kupata uteuzi nne ndani ya mwaka mmoja na msanii wa kwanza wa Afrika anayeongoza kuteuliwa katika kitengo cha 'Best Melodic Rap Performance.'
Pia anakuwa msanii wa kwanza wa Kiafrika kushinda tuzo tano mfululizo za Grammy, ambazo zilianza 2019 hadi 2023.
Mwimbaji wa Marekani Taylor Swift alivunja rekodi ya tuzo za Grammy kwa wimbo wake 'Anti-Hero', na kumfanya kuwa mtunzi wa kwanza wa nyimbo kuwahi kuchaguliwa mara saba katika kitengo cha wimbo bora wa mwaka.
Tuzo za Grammy zitafanyika Februari 4 huko Los Angeles na waandaji bado hawajatangazwa.