Marais wa nchi za ECOWAS wamekashifu hali ambayo rais Mohamed Bazoum ameshikiliwa/ Picha: Others 

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika ameunga mkono maazimo, leo tarehe 11 Agosti, ambayo marais wa jumuiya ya Afrika Magharibi walifikia katika mkutano wao wa kujadili mzozo wa Niger.

Niger imekuwa chini ya mapinduzi ya serikali tangu 26 Julai mwaka huu.

Mapinduzi hayo yamefanywa na wanajeshi.

Kati ya maazimio yao katika mkutano wao wa Ijumaa ilikuwa kuomba nchi za Afrika magharibi kuweka tayari majeshi kwa ajili ya uwezekano wa kutuma majeshi nchini Niger.

"Naunga mkono vikubwa kwa maamuzi yaliyopitishwa na ECOWAS," taarifa kutoa kwa Mahamat Moussa Faki mwenyeiti wa tume ya Umoja Wa Afrika amesema.

Faki ametoa wito kwa mamlaka za kijeshi kuhakikisha kurejea kwa hali ya kikatiba nchini humo na kuachiliwa kwa rais Mohamed Bazoum.

Baadhi ya makubaliano ya marais wa ECOWAS

Rais wa Ivory Coast tayari amesema kuwa nchi yake iko tayari kuchangia majeshi .

Marais pia wamekashifu hali ambayo rais Mohamed Bazoum ameshikiliwa na wanadai kuwa baraza la wanajeshi lina jukumu ya usalama wa rais.

ECOWAS imeapa kuweka juhudi aina yote kuhakikisha suluhu inapatikana Niger.

Marais wameamua kuwa nchi jirani ya Niger zitafunga mipaka yao na nchi hiyo.

Usafiri wa wale wanaoonekana kuunga mkono mapinduzi yatazuiliwa katika eneo hili. Mali ya baadhi ya maafisa Niger yatashikiliwa.

ECOWAS imeomba Umoja wa Afrika ikubaliane na mazimio yao.

TRT Afrika