Bazara la amani na usalama la Umoja wa Afrika halikukubaliana kuhusu kutuma majeshi nchini Niger/ Picha : Umoja wa Afrika 

Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika, lilifanya mkutano kujadili mzozo wa Niger Jumatatu . Mapinduzi nchini humo yalifanyika tarehe 26 Julai na hadi sasa rais Bazoum hajaachiliwa.

Hata hivyo uamuzi juu yake haujatolewa.

Inaripotiwa nchi wanachama zilishindwa kufanya makubaliano ya pamoja kuunga mkono uamuzi wa jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS kutuma wanajeshi Niger kurejesha hali ya kikatiba.

Dkt. Solomon Derrso , Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Amani Afrika, anasema kuwa hakukuwa na matarajio kuwa baraza la amani na usalama lingekubaliana kwa swala la kutuma wanajeshi Niger.

Amani Afrika ni shirika linalofanya utafiti kuhusu maswala ya amani na usalama barani Afrika na linahusiana kwa karibu na baraza la amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

"Wao kutokubaliana imejitokeza kwasababu nchi ambazo hazipo chini ya jumuiya ya ECOWAS haziungi mkono uamuzi wa ECOWAS wa uingiliaji wa kijeshi Niger na zingependelea Niger ipewe adhabu ya kusimamishwa kuhusika na maswala ya AU hadi irejee katika hali ya kikatiba." Dersso anasema.

Mwakilishi wa Niger pia alihudhuria sehemu ya mkutano wa baraza la Amani na Usalama la Umoja wa mataifa Niger/ Picha: Umoja wa Afrika 

Nchi ambazo zipo chini ya mapinduzi ya serikali - Sudan, Mali, Burkina Faso na Guinea zimepigwa marufuku na kukatazwa kuhusika katika mikutano ya aina yoyote ya Umoja wa Afrika , hadi hapo zitakaporejea katika hali ya kikatiba.

Baraza la amani na Usalama la Umoja wa Afrika lina wanachama 15 ambazo ni Burundi, Cameroon, Kongo DRC, Djibouti , Morocco, Namibia, Afrika Kusini, Tanzania , Tunisia , Uganda na Zimbabwe.

Afrika Magharibi ina nchi nne Ghana, Nigeria, Gambia na Senegal.

"Sio kitu kipya kwa baraza la usalama la Umoja wa Afrika kutokubaliana kwa swala fulani, " Derrso anasema ," ni kama tu vile baraza la amani na usalama la Umoja wa mataifa hutofautiana kwa maswala tofauti , hii ni kawaida kwa tume hizi ambazo ni muhimu kwa uamuzi."

Mkutano huo ulifanyika huku viongozi wa mapinduzi nchini Niger wakitishia kumhukumu rais Mohamed Bazoum kwa makosa ya uhaini .

Jumuiya ya ECOWAS ilipotangaza kuwa imeamua kutuma wanajeshi Niger baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika halikutamka kuiunga mkono.

"Ni vizuri pia kwa baraza hili kutofautiana hivyo, " Derrso anasema, " inamaanisha kuwa kuna mifumo ya kuangalia makosa na changamoto ya maamuzi tofauti katika tume hii ya kibara,"

Katiba ya Umoja wa Afrika halina vipengele vya kuongoza uingiliaji wa kijeshi katika nchi yoyote ya Afrika kwa ajili ya kupigana na waliofanya mapinduzi.

wasiwasi wa AU uko wazi kabisa

TRT Afrika