Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC) kimesisitiza kuwa bado bala la Afrika halijaweza kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Mpox.
“Kwa sasa, tunaweza kusema kuwa bara la Afrika bado halijaweza kuudhibiti ugonjwa wa Mpox,” alisema Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Afrika CDC amesema katika mkutano wa mtandaoni.
Ukilinganisha na kipindi kama hiki kwa mwaka jana, Kaseya amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la asilimia 177 na 38.5 katika idadi ya maambukizi na vifo mtawalia, katika nchi 15 barani Afrika.
Kulingana na Kaseya, kumekuwepo na maambukizi mapya 2,912 katika wiki za hivi karibuni, na vifo 14, huku akisisitiza haja ya kuongeza na kuimarisha njia za uchunguzi na udhibiti wa ugonjwa huo.
Bara la Afrika lina jumla ya maambukizi 29,000 na vifo 738 mwaka huu, kwa mujibu wa Afrika CDC.
Kaseya, pia amegusia changamoto za uhaba wa vifaa vya kupimia ugonjwa huo.
“Tuzungumzie chanjo. Tumeona mafanikio nchini Rwanda, ambako watu 500 wameshapata chanjo hiyo,” alisema Kaseya.
Rwanda imepokea dozi 1,000 za chanjo hiyo kutoka Nigeria chini ya mkataba wa nchi mbili, kutoka dozi 10,000 ambayo ilipokea kutoka Marekani.