Kwa mara ya kwanza, vitabu vya kiada vya lugha ya Kiarabu na Elimu ya Dini ya Kiislamu (IRE) vimechapishwa pia na kuzinduliwa nchini Sudan Kusini.
“Kuzinduliwa kwa Lugha ya Kiarabu na Elimu ya Dini ya Kiislamu ni mafanikio, inathibitisha dhamira ya kutoa elimu bora kwa wote," Hussein Abdelbagi Akol, makamu wa rais wa kitengo cha utoaji huduma katika Jamhuri ya Sudan Kusini alisema.
"Kutakuwa na changamoto katika ufundishaji wa kitabu hiki iwapo hatutakuwa na walimu wa kutosha, hivyo naihimiza Wizara ijikite katika kuhakikisha wanapatikana walimu wa kufundisha lugha ya Kiarabu na Elimu ya Dini ya Kiislamu," alisema Akol.
Vitabu hivyo ni kati ya zaidi ya vitabu milioni 2.5 vya kiada vilivyokabidhiwa kwa viongozi wa shule mjini Juba kama sehemu ya mpango mkubwa unaolenga kuhakikisha watoto ambao hawajaenda shule wanaweza kupata elimu nchini Sudan Kusini.
Mpango huo ni mojawapo ya mipango ya ufadhili wa elimu nchini Sudan Kusini unaoongozwa na Save the Children kwa ushirikiano na Baraza la Wakimbizi la Norway, Finn Church Aid, na Wizara ya Elimu ya Jumla na Maelekezo (MoGEI), na kufadhiliwa na mpango wa Education Cannot Wait (ECW).
Usambazaji huu wa hivi majuzi wa vitabu milioni 2.5 unaongeza vitabu vya kiada milioni 1.12 vilivyosambazwa tayari, na kufanya jumla ya vitabu zaidi ya milioni 3.5 vilivyosambazwa tangu 2021.
Inakadiriwa kuwa watoto milioni 2 wakimbizi wa ndani na wanaorejea nyumbani, pamoja na walimu 41,000, wote wanahitaji misaada ya kibinadamu inayohusiana na elimu nchini Sudan Kusini.
Mahitaji haya ni tofauti na yanahitaji uingiliaji wa kina, wa sekta nyingi, haswa katika maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa. Ukosefu wa vifaa vya kutosha vya kufundishia mfano vitabu vya kiada kumechangia watoto hao huku wasichana wakiwa asilimia 53 wakikabiliwa na vikwazo vikubwa vya kupata elimu.
“Vitabu milioni 2.5 ambavyo tunasambaza shuleni leo asubuhi vitachangia kupunguza uwiano wa vitabu vya wanafunzi. Nilipokuja ofisini, ilikuwa ni mwanafunzi kati ya mwanafunzi mmoja na19 kwa kila kitabu katika masomo ya msingi kama vile lugha ya Kiingereza na Hesabu," alisema Awut Deng Achuil, Waziri wa Elimu ya Jumla na Maagizo katika Jamhuri ya Sudan Kusini.
"Leo, ni wanafunzi watatu kwa kila kitabu; hii haitoshi; lengo langu ni mtoto mmoja wa shule kwa kila kitabu,” alisema Achuil.
Watalamu wanasema watoto wenye ulemavu, hasa wale walio katika maeneo yaliyoathiriwa na mgogoro, wanaendelea kukosa msaada wa kutosha wa kujifunza kwa ajili ya elimu bora.