Salva Kiir elections

Serikali ya Sudan Kusini imeamua kuahirisha uchaguzi wa kitaifa uliocheleweshwa kwa muda mrefu hadi Desemba 2026, ofisi ya rais ilisema Ijumaa, ikisisitiza changamoto zinazokabili mchakato tete wa amani nchini humo.

“Ofisi ya Rais, chini ya uenyekiti wa Rais Salva Kiir Mayardit, imetangaza kuongeza muda wa mpito wa nchi hiyo kwa miaka miwili pamoja na kuahirisha uchaguzi ambao awali ulipangwa kufanyika Desemba 2024 hadi Desemba 22, 2026,” ilisema ofisi ya Kiir kwenye Facebook.

Sudan Kusini kimsingi imekuwa na amani rasmi tangu mkataba wa 2018 uliomaliza mzozo wa miaka mitano uliosababisha mamia kwa maelfu ya vifo, lakini ghasia kati ya jamii hasimu huchipuka mara kwa mara.

Hadi tangazo la Ijumaa, lilikuwa linapanga kuchagua viongozi watakaorithi serikali ya mpito ya sasa, ambayo ni pamoja na Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar, ambao vikosi vyao vilipigana wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

"Kuna haja ya muda wa ziada kukamilisha kazi muhimu kabla ya uchaguzi," ofisi ya Kiir ilisema.

Raia wa Sudan Kusini wana hamu ya kushiriki katika uchaguzi wa kwanza baada ya uhuru. Uchaguzi wa mwisho, ulifanyika Machi 2010, ulishuhudia Rais aliyeko madarakani Salva Kiir akishinda kwa zaidi ya asilimia 90.

TRT Afrika na mashirika ya habari