Rais wa Somalia Mohamud akiwa na Mkuu wa Jeshi Somalia wakati wa sherehe ya maadhimisho ya Uhuru | Picha: Villa Somalia

Mikoa ya kusini ya Somalia ilijinyakulia uhuru kutoka kwa wakoloni wa Italia mnamo 1960 baada ya miaka kadhaa ya mapambano huku mikoa ya kaskazini, ambayo sasa ni Somaliland, ikipata uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo Juni 26, 1960, na kuungana na Kusini siku nne baadaye na kuwa Jamhuri ya Somalia.

Akiongoza sherehe hizo mapema siku ya Jumatatu, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitumia hotuba yake kutoa wito wa umoja na amani huku akiwapongeza raia wa nchi hiyo kwa maadhimisho hayo.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud | Picha: Villa Somalia

“Hongera, hongera. Natoa pongezi kwa raia wote wa Somalia walioko ndani na nje ya nchi tukisheherekea miaka 63 tangu bendera hii yetu iliposimamishwa. Kwa hakika tunajivunia juhudi za mashujaa wetu walitunyakulia uhuru wetu.” Alisema rais Hassan Sheikh.

Aidha Rais Hassan Sheikh Mohamud, ambaye aliongoza sherehe hiyo iliyoandaliwa katika makao makuu ya Mamlaka ya Benadir, jijini Mogadishu, aliwashauri viongozi na watu wanaoshikilia nyadhifa za uongozi katika viwango mbalimbali kueneza amani na kutowaganya wananchi kama njia ya kufanikisha amani na maendeleo.

“Viongozi nawaomba, muwe katika mstari wa mbele kuwaleta Pamoja wananchi katika maeneo yenu. Muwape sikio wananchi na muwajumuishe katika taratibu zote za kuleta amani na umoja ili tuyatimize malengo yetu kama taifa kwa Pamoja.” Aiongeza.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud | Picha: Villa Somalia

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu Salah Jama na maspika wa mabunge yote mawili; Spika wa Seneti Abdi Hashi Abdullahi na Spika wa Bunge Aden Madobe.

TRT Afrika