Mamlaka

Mamlaka za mji mkuu wa Sierra Leone zimesema kuwa zitaanza kutumia polisi wenye silaha kulinda makaburi hayo kufuatia wizi wa mifupa kutoka kwa miili iliyozikwa eneo hilo.

Wizi wa mifupa ya binadamu unahusishwa na utengenezwaji wa "kush", dawa yenye nguvu kama bangi, afisa kutoka halmashauri ya jiji la Freetown ameliambia shirika la habari la AFP, KWA masharti ya kutotajwa jina.

Dawa hiyo imejizoelea umaarufu kati ya vijana katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ingawa utengenezwaji wake bado haujawekwa bayana.

Madai kwamba dawa hiyo ya kulevya imetengenzwa na mifupa ya binadamu iliyosagwa yameripotiwa katika vyombo vya habari vya nchi hyio, japo bado hayajathibitishwa kisayansi.

"Halmashauri ya jiji la Freetown imepata taarifa za baadhi ya wenye nia ovu dhidi ya ndugu zetu marehemu ," imesema mamlaka hiyo katika taarifa yake ya Jumanne.

Halmashauri hiyo ilitangaza, "Kuweka katazo la watu kupita maeneo ya makaburini kuanzia saa moja usiku kila siku; hakuna mtu atakayeruhusiwa kupita au kufanya shughuli yoyote katika eneo la makaburi".

Iliongeza "wakati wote, maeneo yote yatakuwa yanalindwa na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale watakaokaidi agizo hilo.

Taarifa ya idadi ya polisi na maeneo yalioathirika na wizi huo hazikuweza kuthibitika mara moja, kulingana na chanzo za polisi

Maofisa wa mji huo wamewaasa wakazi waishio karibu na makaburi hayo kuwa macho na kutoa taarifa kwa polisi juu ya uwepo wa watuhumiwa hao.

TRT Afrika