Ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda./Picha: Getty

Shirika la Ndege la nchini Rwanda, RwandaAir limetangaza kusitisha safari zake za kwenda mji wa Cape Town ulioko Afrika Kusini.

Katika uamuzi wake, RwandaAir imeweka bayana kuwa hakutokuwa na safari za ndege ya shirika lake kuelekea mji huo wa bandari, kuanzia Oktoba 27, 2024.

Licha ya kusitisha safari za kwenda Cape Town, shirika hilo linafanya safari katika mjini 18 barani Afrika, ikiwemo Johannesburg.

“Abiria wote wenye tiketi za safari za kuanzia tarehe tajwa wanapaswa kuwasiliana na sisi mapema iwezekanavyo,” lilisema Shirika hilo katika ukurasa wake wa X.

TRT Afrika