Juhudi za kwanza za  kubadilisha majina ya mitaa na alama muhimu zilianzia miaka ya 1970.  /Picha: Reuters

Na Firmain Eric Mbadinga

Historia inajuridia katika baadhi ya nchi zinazotaka kubadilisha majina ya miji, mitaa na maeneo muhimu kwa sababu mbalimbali, mara nyingi ili kurejesha utambulisho wa kitamaduni wa taifa au kuthibitisha uhuru wake.

Mabadiliko haya mara kwa mara huja kutokana na mabadiliko makubwa ya kijamii na kisiasa, kama vile mwisho wa utawala wa kikoloni, kupinduliwa kwa utawala, au kuunganishwa kwa eneo.

Mamlaka za kijeshi nchini Mali, Burkina Faso na Niger zimeendelea na mipango yao ya kubadilisha majina ya mitaa katika miji yao mingi katika harakati zao za kutafuta utambulisho na ukombozi.

Mkuu wa kijeshi wa mpito wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré, mwenzake wa Niger Abdourahamane Tchiani, na Jenerali Assimi Goita wa Mali wote wameamua kuondoa majina ya majenerali na vigogo wa kisiasa wa enzi ya ukoloni wa Ufaransa katika majengo na mitaa.

Majina maarufu ya Kifaransa kama vile Charles de Gaulle, Louis Faidherbe na Michel de Montaigne ni miongoni mwa yale yaliyofutwa katika nchi za Muungano wa des États du Sahel (Muungano wa Majimbo ya Sahel).

Kumekuwa na mvutano kati ya nchi hizo tatu na Ufaransa. Wanamtuhumu mtawala huyo wa zamani wa kikoloni kwa uvunjifu wa amani wa kisiasa na kimaeneo.

Upinzani unaoongezeka

Mnamo 2022, waziri wa mambo ya nje wa Mali, Abdoulaye Diop, aliufahamisha Umoja wa Mataifa kwamba nchi yake inaweza "kutoa ushahidi wa vitendo vya kijasusi na kuvuruga utulivu vinavyofanywa na Ufaransa".

Hivi majuzi, nchi hizo tatu zilitoa kauli kama hizo zikisisitiza madai ya kutumiwa kwa jumuiya ya kikanda ya ECOWAS na Ufaransa kwa lengo la kuvuruga mifumo yao ya kiuchumi.

Huku mchakato wa 'kuweka majina ya Kiafrika' kwenye mitaa na maeneo muhimu ukishika kasi, Burkina Faso inataja utajiri wa urithi wa Kiafrika kama sababu ya kuzipa maeneo yenye majina ya Kifaransa utambulisho mpya.

Mnamo Oktoba 2023, jina la Boulevard Charles de Gaulle katika mji mkuu wa Ouagadougou lilibadilishwa na kupewa jina rasmi la Boulevard Thomas Sankara baada ya Rais wa zamani wa nchi hiyo kuuawa.

Kuongezeka kwa hisia za chuki dhidi ya Ufaransa kulisababisha kufukuzwa kwa wanajeshi wa Ufaransa katika eneo la Sahel. /Picha: Wengine

Zaidi ya mwaka mmoja baadaye, Niger ilibadilisha jina la Avenue Charles de Gaulle kwa jina la Niamey baada ya Djibo Bakary, mtu muhimu aliye pigania uhuru wa nchi hiyo.

Mali ilifuata mkondo huo mnamo Desemba 19, na kubadilisha jina la Avenue de la Cedeao (kifupi cha Kifaransa cha ECOWAS) huko Bamako kwa AES, kukamilisha mzunguko wa mabadiliko.

Mitazamo tofauti

Uwanja wa jadi wa nchini Mali ulioko mbele ya Bunge la Kitaifa unaonyesha Mali ya zamani, na uwakilishi wa wasanii na dini, sawa na Msikiti maarufu wa Djenné.

L'obélisque des idéogrammes huko Bamako ina maandiko maarufu ya Sundiata Keita kwa lugha ya Nko inayosema, "Boti ya Mali inaweza kutikisika, lakini haitapinduka kamwe."

Tchanga Chérif Tchouloumbo, mwanafunzi kutoka Niamey, anaonekana kutojali.

Anaamini ya kwamba kushughulikia masuala muhimu ya nchi inapaswa kutangulizwa kuliko kubadilisha majina ya mitaa na alama nyingine muhimu.

Tchouloumbo na Doumbia wana wasiwasi zaidi kuhusu uwezo wa viongozi wao kuboresha usalama na kuhakikisha usalama.

Naye, Issa Ibrahim Alou kutoka Niamey anakubaliana na mchakato huo katika nchi yake, Mali na Burkina Faso.

"Sisi, Jumuiya ya Maendeleo ya Vijana wa Niger, tumekuwa tukitaka hatua kama hii. Sasa inafanyika, tunaiona kama jambo zuri. Tunazipongeza mamlaka za mpito kwani mchakato huu ni sehemu ya mapambano ya uhuru wetu," anaiambia TRT Afrika.

Kapteni wa Burkina Faso Ibrahim Traoré, Abdourahamane Tchiani wa Niger, na Jenerali Assimi Goita wa Mali walitia saini mkataba wa kuunda Muungano wa Nchi za Sahel mwaka 2023. Picha: Wengine

Zaidi ya mipaka ya jiografia

Dk Massamba Guèye, mtafiti, mwandishi na mwanzilishi wa Maison de l'Oralité et du Patrimoine yenye makao yake mjini Dakar nchini Senegali, anaamini kuwa ni suala linalovuka tawala au migawanyiko ya kijiografia.

Anaamini mada hiyo inapaswa kushughulikiwa kimsingi kutoka kwa mtazamo wa utambulisho na urithi wa kitamaduni "Kwa maoni yangu, wakoloni hawapaswi kuchukuliwa kama mashujaa katika bara la Afrika.

Mtaa unapopewa jina la mhusika, ni kwamba vizazi vipya lazima vimchukulie kama kielelezo.

Itakuwa haifai kumchukulia mtu ambaye aliwafanya mababu zetu kuwa watumwa kama kielelezo," anasema Dk Guèye.

"Kwa kazi halisi ya utengenezaji wa kumbukumbu, itakuwa muhimu kuhusisha idadi ya watu na kuhakikisha kuwa barabara inapobadilishwa jina, inapatiwa jina lake la asili. Pia itakuwa muhimu kuweka alama ya kufuta majina ya kipindi cha ukoloni."

Juhudi za kwanza za kubadilisha jina zilianzia miaka ya 1970, huku Rais wa zamani Mobutu Sese Seko wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiachana na jina lake la kwanza la Kimagharibi, Joseph-Désiré.

Nyumba na maeneo ya umma pia yalihitaji kuwa na majina ya Kiafrika.

Kiongozi maarufu wa Pan-Africanist Kapteni Thomas Sankara alipanda mbegu ya Uafrika kwa kubadilisha jina la nchi yake, wakati huo iliitwa Upper Volta, hadi kuitwa Burkina Faso.

Mchambuzi wa kisiasa na kiusalama Mubarak Aliyu anaamini kuwa mwelekeo huo unatokana na mambo mawili makuu - ushirikiano wa kiuchumi wa upande mmoja kati ya Ufaransa na makoloni yake ya zamani na ushawishi wa kijeshi wa Ufaransa katika baadhi ya nchi.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika