Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametumia kipengele 97 cha katiba ya nchi kutoa msamaha kwa wafungwa. Picha: Reuters

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesamehe wafungwa 588 katika magereza mbalimbali ya nchi.

Miongoni mwa wafungwa waliosamehewa ni pamoja na wazee 11 na mama mwenye mtoto, vyombo vya habari vya ndani vimemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ulinzi Jack Mwiimbu.

Kifungo cha maisha kimepunguzwa hadi miaka 35 na wafungwa wawili ambao awali walihukumiwa kifo hivi sasa watafungwa maisha, waziri aliwaambia waandishi wa habari mjini Lusaka siku ya Jumapili.

Kusamehewa kwa wafungwa na Rais Hichilema ilikuwa ni utekelezaji wa kifungu nambari 97 cha katiba ya nchi ambacho kinampa rais mamlaka ya kusamehe au kubadilisha adhabu iliyowekwa kwa wafungwa, amesema Waziri Jack Mwiimbu.

Amesema msamaha huo umeonyesha tabia nzuri baada ya wafungwa kujirekebisha tabia ambayo itawasaidia kujumuika na jamii.

TRT Afrika