Rais Erdogan amesema kuwa Uturuki iko pamoja na wa watu wa Libya. Picha: AA

Rais Erdogan, kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, aliwaombea na kuwatakia rehema za Mwenyezi Mungu wale wote waliopoteza maisha kutokana na janga la mafuriko nchini Libya na uponyaji wa haraka kwa waliojeruhiwa.

Erdogan, kwenye ujumbe wake wa kuwatakia watu wa Libya "wapone haraka", alisema Uturuki iko pamoja na watu wa Libya. Chini ya uratibu wa AFAD yetu, ndege 3 zimepangwa kutua Benghazi asubuhi ya leo." aliandika.

"Kwanza, wafanyakazi 168, magari 2 ya utaftaji na uokoaji, boti 2 za uokoaji zitakuwa kwenye ndege yetu kusaidia shughuli za uokoaji na zingine; mahema 170, blanketi 600, vifurushi 400 vya chakula na usafi, jenereta 20, jaketi 1000 ya kuzuia mvua, buti 500 na tochi 500 zitatolewa kwa harakati zote na zingine." alieleza kwa taarifa yake.

Aidha, Rais Erdogan aliongeza kuwa AFAD, pamoja na watalaam wengine kutoka Kurugenzi kuu ya usalama watashiriki katika harakati za uokoaji, Erdogan alisema.

" Wafanyakazi wetu ni pamoja na kikosi cha utafutaji na uokoaji majini na juu ya maji inayojumuisha watu 65, wanachama wa mwezi mwekundu, UMKE na mashirika mengine ya kushiriki katika usanikishaji na usambazaji wa makazi ma misaada ya kibinadamu." alimaliza.

AA