Nigeria imepokea helikopta nne kati ya sita zilizotengenezwa nchini Uturuki./Picha: AA

Mwisho wa magaidi nchini Nigeria, baada ya nchi hiyo kununua vifaa vya kijeshi kutoka nchini Uturuki, Waziri wa Ulinzi wa Nigeria Mohammed Badaru Abubakar amesema.

Abubakar alitoa kauli hiyo katika kambi ya jeshi la anga la Nigeria (NAF) katika jimbo la Katsina, wakati wa kuzindua kwa helikopta mbili aina ya T129 ATAK, ambazo zimenunuliwa kutoka Uturuki.

"Mwisho wa magaidi hapa nchini umekaribia ," alisema Waziri huyo mapema wiki hii.

Pia amelitaka Jeshi la Anga kushirikiana na vikosi vya ardhini na wadau wengine kupambana na maadui wa taifa hilo.

Nigeria ilizindua helikopta hizo wiki hii./Picha: Wengine

Helikopta mbili aina ya T129 ATAK zilizopokelewa mwezi Septemba, zimeimarisha mapambano dhidi ya vikundi vyenye silaha, alisema waziri huyo.

Uhusiano unaokua

Nigeria ilikubaliana na kampuni ta Uturuki ya TAI kununua helikopta sita aina ya T-129 ili kuimarisha uwezo wake wa ulinzi wa anga.

Ushirikiano wa kijeshi na wa kiuchumi kati ya Nigeria na Uturuki unazidi kukua, huku nchi hizi zikitarajiwa kutiliana saini mkataba mwingine wa kiulinzi wenye thamani ya zaidi dola bilioni 2.

TRT Afrika