Niger inazalisha asilia mia 5 ya urani ya dunia / picha Reuters 

Niger ni kati ya nchi zinazozalisha viwango vikubwa vya urani yaani uranium duniani.

Inazalisha asilimia 5 ya urani ya dunia. Ilizalisha tani 2,020 za madini haya mnamo 2022.

Uranium inatoa mafuta yanayotumika sana kwa nishati ya nyuklia, silaha za nyuklia, vitu vya kinyuklia ambavyo vinasaidia kuendesha meli pamoja na nyambizi.

Niger ina migodi mitatu ya urani / Picha : reuters 

Ufaransa inanunua Uranium kutoka Niger kwa ajili ya mitambo yake ya nyuklia.

Niger ina migodi mitatu ya urani.

Katika migodi ya Arlit kampuni ya Ufaransa ya Orano ndiye mwendeshaji wa uchimbaji wa Urani na inamiliki 63.4% ya migodi. Kampuni ya serikali ya Niger inayoitwa National des Resources Minières du Niger (ONAREM) inamiliki 36.6%.

Katika mgodi ya Akouta Niger ilizalisha tani 75,000/ picha Reuters 

Katika mgodi ya Akouta Niger ilizalisha tani 75,000 ya uranium kutoka mwaka 1978 hadi Mach 2021 kabla ya mgodi huu kufungwa. Kampuni ya Ufaransa ya Orano ilikuwa ilimiliki 59%.

Kampuni ya serikali ya Niger SOPAMIN ilikuwa na 39% huku kampuni ya Enusa (Spain) ikimiliki 10%.

Ufaransa inanunua Uranium kutoka Niger kwa ajili ya mitambo yake ya nyuklia/ Picha Reuters 

Katika mgodi wa IMOURAREN leseni ya operesheni ilitolewa mwaka 2009 lakini uchimbaji wa uranium ulisimamishwa mwaka 2014 kwa ajili ya kungoja soko la Uranium duniani iwe bora zaidi.

Kampuni ya ufaransa ya Orano inamiliki asilimia 63.52% na kampuni ya NIger ya Sopamin ya Niger ina 33.35%.

Mwezi mei mwaka huu kampuni ya Ufaransa ya Orano ilisaini makubaliano na serikali ya Niger kuchimba Uranium hadi mwaka 2040.

Viongozi wa mapinduzi ya serikali ambao walimuondoa rais Mohamed Bazoum 26 julai mwaka huu bado hawajagusia swala la kandarasi ya Ufaransa kuendelea kuchimba Urani nchini humo.

TRT Afrika