Mnamo Machi 2021, wakati rais Mohamed Bazoum alipokuwa karibu kuapishwa baada ya uchaguzi, Jenerali Abdourahamane Tchiani anasifiwa kwa kuongoza kitengo kilichozuia jaribio la mapinduzi nchini Niger.
Lakini sasa mambo yamegeuka, amempokonya uongozi yule ambaye alilinda wakati huo.
Licha ya kuongezeka kwa wito wa yeye kurudisha serikali kwa rais Mohamed Bazoum na hata tishio la hatua za kijeshi za mataifa jirani ya Afrika Magharibi, Jenerali Abdourahamane Tchiani anaendelea kujiimarisha kama kiongozi mpya wa Niger.
Tchiani, 62, anatoka eneo la Tillaberi magharibi mwa Niger, ambalo linapakana na Mali.
Akiwa anatoka katika kabila kubwa la Wahausa, kituo cha kuajiri jeshi, ana taaluma ya kijeshi ya takriban miaka 40.
Tchiani alihudhuria vyuo vya kijeshi nchini Ufaransa, Marekani, Senegal, Morocco na Mali, huku akipanda vyeo bila uhusiano wowote wa wazi wa kisiasa.
Ameshikilia nyadhifa kadhaa za kamandi nchini Niger, huku pia akiwa sehemu ya operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast, jimbo la Darfur nchini Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Pia alihudumu kama mjumbe wa kijeshi katika Ubalozi wa Niger nchini Ujerumani. Mnamo 2011, aliteuliwa kuwa mkuu wa walinzi wa rais, kitengo maalum cha wanajeshi wapatao 2,000, na rais wa zamani Mahamadou Issoufou, mtangulizi wa Bazoum.
Alipandishwa cheo na Issoufou hadi cheo cha jenerali mnamo 2018.
Mnamo Machi 2021, wakati Bazoum alipokuwa karibu kuapishwa baada ya uchaguzi, Tchiani anasifiwa kwa kuongoza kitengo kilichozuia jaribio la mapinduzi nchini Niger.
Je, Jenerali Abdourahamane Tchiani atarejesha serikali?
Jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS imeamua kutuma wanajeshi nchini Niger , kwa ajili yakurudisha hali ya kikatiba .
Rais Mohamed Bazoum bado ameshikiliwa na viongozi wa mapinduzi tangu 26 Julai huku jamaa zake wakisema kuwa anashikiliwa kwa hali mbaya.
Jenerali Abdourahamane Tchiani, ambaye aliongoza mapinduzi ya Julai 26 dhidi ya rais Mohamed Bazoum, amewasilisha dhamira yake kwa kuzindua serikali ya mpito, akimtaja Ali Lamine Zeine kuwa waziri mkuu na Baraza la Mawaziri lenye watu 21.
Tayari kuna utata hasa kwa hali ya usalama wa rais Bazoum na nchi ya Sahel ikiwa wanajeshi wataingia nchini humo.
Mkutano wa viongozi wa kijeshi wa Afrika Magharibi ulipoangwa kufanyika 12 Agosti haujafanyika,
Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika limepanga kukutana tarehe 14 Agosti , kujadili swala la Niger .
Jumuiya ya ECOWAS imeomba Umoja wa Afrika kukubali maazimio yao yote ya mkutano wa marais ambao ulipendekeza majeshi kutumwa Niger.
Lakini wataalam wa maswala ya kikanda na usalama wanasema ni muhimu kwa majorani wa Niger kuzingatia kuwashawishi viongoizi wa Mapinduzi nchini Niger kufanya mazungumzo na kuelewa umuhimu wa kurejesha upongoiz wa raia.
Hofu ingine ya usalama ni kwamba nchi za Mali na Burkina Afaos na Guinea ambazo pia ziko chini ya uongozi wa kijeshi zimeapa kutetea Niger ikiwa wanajeshi wowote watatumwa katika nchi hiyo.