Jenerali Abdourahamane Tchiani ameonekana kwenye televisheni ya taifa kama kiongozi mpya wa Niger/ Picha  : AP

Mkuu wa walinzi wa rais wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, ameonekana kwenye televisheni ya taifa siku ya Ijumaa akikaa kama rais wa baraza la mpito lililonyakua mamlaka katika mapinduzi.

Kikundi cha walinzi wa rais walifanya mapinduzi siku ya Jumatano na kumweka kizuizini rais Mohamed Bazoum.

Abdourahamane Tchiani alikariri kuwa wanajeshi walichukua madaraka kutokana na hali mbaya ya usalama nchini.

Pia alikosoa kutoshirikiana na serikali za kijeshi nchini Burkina Faso na Mali katika mapambano dhidi ya waasi eneo hilo.

Niger ni muhimu kwenye mapambano ya kimataifa dhidi ya waasi katika Afrika Magharibi na idadi ya askari wa kigeni wanakaa huko.

Rais Mohamed Bazoum hajaonekana hadharani tangu wanajeshi walipozingira ofisi yake siku ya Jumatano.

Lakini kitendo cha wanajeshi hao kimezua shutuma za kimataifa na shinikizo linazidi kuwataka wamuachilie huru Rais Bazoum ambaye wamemzuia.

Ufaransa yasema mapinduzi "hayajakwisha"

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna amesisitiza kuwa mapinduzi nchini Niger bado hayakuwa ya "mwisho" na kuelezea matumaini yake kwamba wapangaji njama ambao wamemzuilia rais watatii wito wa kimataifa wa kurejeshwa kwa utawala wa kidemokrasia.

Rais Bazoum Mohamed amezuiliwa na wanajeshi tangu Jumatano / Photo: AP

"Ikiwa unanisikia nikizungumza kuhusu jaribio la mapinduzi, ni kwa sababu hatuzingatii mambo ya mwisho, bado kuna njia ya kutoka ikiwa wale waliohusika watasikiliza jumuiya ya kimataifa," Colonna alisema Ijumaa.

Ufaransa iliyo na wanajeshi 1,500 nchini Niger, awali ilitoa wito wa "kurejeshwa kwa uadilifu wa taasisi za kidemokrasia za Niger," shirika la habari la AFP linaripoti.

Mkuu wa majeshi ya Niger Jenerali Abdou Sidikou Issa ameegemeza uzito wake nyuma ya waliopanga mapinduzi.Lakini kumekuwa na shinikizo la kimataifa kwa wanajeshi nchini Niger kuachana na jaribio la mapinduzi na kuruhusu miundo ya kidemokrasia kufanya kazi.

UN kuchukua hatua

Marekani inasema inaunga mkono hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kupunguza hali ya mambo nchini Niger, msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa alisema Alhamisi, shirika la habari la Reuters linaripoti.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alizungumza na rais wa Niger, Mohamed Bazoum, siku ya Alhamisi, kulingana na usomaji wa Marekani.

"Ameeleza kuwa Marekani iko imara katika kuunga mkono demokrasia ya Niger na inaunga mkono kuchukua hatua katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupunguza hali hiyo, kuzuia madhara kwa raia, na kuhakikisha utaratibu wa kikatiba," msemaji alisema.

Kumekuwa na hali ya utulivu katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika tangu Jumatano wakati baadhi ya wanachama wa Walinzi wa Rais walipompinga Rais Bazoum kuziba ofisi yake na kumweka kizuizini.

Siku ya Alhamisi, baadhi ya waandamanaji walifanya vurugu wakichoma moto mwingi katika makao makuu ya chama tawala katika mji mkuu Niamey.

TRT Afrika