Uongozi wa kijeshi nchini Niger ambao ulichukua uongozi kufuatia mapinduzi, unaripotiwa kumtaka Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia masuala ya kibinadamu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuondoka Niger ndani ya saa 72.
Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa yake ya Jumanne kwamba serikali ilimuamuru Louise Aubin, "kuchukua hatua zote zinazohitajika kuondoka Niamey ndani ya saa 72."
Ufaransa siku ya Jumanne ilianza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Niger pamoja na kuwahamisha maafisa wa kidiplomasia baada ya wiki kadhaa za vuta ni kuvute na watawala wa kijeshi .
Wanajeshi wa nchi hiyo walimuondoa rais aliyekuwa madarakani Mohammed Bazoum tarehe 26 Julai, 2023.
TRT Afrika