Na Kudra Maliro
Iliyoundwa kwa mtindo wa usanifu wa Sudan, Msikiti Mkuu wa Mopti, unaojulikana kama Msikiti wa Komoguel, unachukua eneo la mita mraba 12 hadi 76.
Msikiti ulio katikati mwa Mali ulijengwa kati ya 1933 na 1935. Ulichukua nafasi ya msikiti wa awali uliojengwa mwaka 1908.
Msikiti Mkuu wa Mopti ulikuwa katika hali ya hatari ndipo wakfu wa utamaduni wa Aga Khan Trust for Culture ilipoombwa kuukarabati.
Kwa miaka mingi ilinusurika kutokana na jamii iliyoidumisha kwa kuipaka kwa udongo na majani ya mpunga. Kila mwaka, watu kadhaa kutoka mji wa Mopti hukusanyika ili kuuvisha msikiti vazi jipya la matope.
Amadou Ba, mwenye umri wa karibu miaka 45, amekuwa akishiriki katika hafla ya kukarabati msikiti huo tangu alipokuwa mdogo.
Fahari ya kitamaduni
"Ni babu yangu ndiye aliyenileta kwa mara ya kwanza kushiriki katika sherehe hii. Nilikuwa na umri wa miaka minane pekee wakati huo. Tulisoma Kurani tukufu na tukafunikwa kabisa na matope," Amadou Ba anaiambia TRT Afrika.
Bw Ba, kama wengine wengi kutoka Mopti, amesafiri umbali mrefu kushiriki katika mila hii ya duara, akiongeza kuwa msikiti huo ni fahari ya kitamaduni ya mji huo.
"Ninaishi Bamako kwa sasa, lakini siwahi kukosa sherehe hii," asema mtoto wa kiume wa Mopti mwenye umri wa miaka 45.
Likiwa na urefu wa mita 31, upana wa mita 17 na urefu wa mita 15, lilijengwa kwa matofali ya banco na kupigwa lipu kwa nyenzo hiyohiyo. Inajumuisha sehemu mbili: ya kwanza imefunikwa na ya pili ni ua.
Jengo hilo limezungukwa na ukuta wa mzunguko wenye urefu wa kati ya mita 2.40 na 2.90. Paa inategemezwa na nguzo kubwa zilizopangwa sambamba na ukuta wa Qibla (dalili ya mwelekeo wa Makka).
Fursa ya kuwakutanisha watu
Kwa Bw Ba, tukio hili sio tu la kurejesha msikiti, lakini pia la kuleta pamoja familia na marafiki wanaoishi mbali na Mopti.
Msikiti wa Komoguel unakaribisha idadi kubwa zaidi ya waumini huko Mopti wakati wa sala, haswa wakati wa sala ya Ijumaa.
Tabia hii ya kuunganisha hufanya mnara huu wa kidini kuwa chombo cha kudumisha na kuimarisha mahusiano ya kijamii.
Amadou N'diaye, mhusika mkuu wa eneo hilo, anaamini kwamba kwa utamaduni huu wa kila mwaka wa kurejesha Mopti, jengo hilo daima litabaki kuwa ishara ya fahari.
Kulingana na takwimu za Wizara ya Masuala ya Kidini na Ibada, Waislamu ni karibu 95% ya wakazi nchini Mali. Msikiti huo una umuhimu wa kihistoria, usanifu, kiutamaduni na kiroho na ni kivutio kikubwa kwa watalii.
“Natumai mila hii itaendelea kupitishwa kutoka kizazi hadi kizazi... Tutegemee wajukuu na vitukuu zangu pia watashiriki katika ukarabati wa msikiti,” anamalizia Bw N’diaye.