Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan ametembelea maonesho ya "Safari ya mapishi ya ladha ya karne ya Anatolia" pamoja na wake wa viongozi wengine waliohudhuria Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya.
Katika toleo lake la tatu, Mkutano umeleta pamoja viongozi wa nchi na serikali, mawaziri, wanadiplomasia, wafanyabiashara, wasomi, wabobezi, na majopo mbalimbali na maonesho yaliyohusisha masuala mbalimbali.
Mkutano huo ukiingia siku yake ya pili Jumamosi, umehodhi maonesho ya "Safari ya mapishi ya ladha ya karne ya Anatolia", ukitoa fursa kwa washiriki kuona bidhaa zenye alama ya kijiografia na bidhaa za mkono.
Mke wa Rais wa Uturuki ametembelea maonesho pamoja na Rais wa zamani wa Croatia Kolinda Grabar Kitarović, mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini (TRNC) Zerrin Ustel, mke wa rais wa TRNC Sibel Tatar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Grace Naledi Mandisa Pandor, na mke wa Rais wa Serbia Tamara Vucic.
Mke wa Rais wa Uturuki na viongozi alioandamana nao alitoa elimu kuhusu mavazi na vitu vyengine vya kitamaduni, pamoja na rangi.
Wageni pia walitembelea vibanda vinavyoonesha bidhaa za kijiografia zenye ithibati kutoka Umoja wa Ulaya, wakati mke wa Rais wa Uturuki akiandamana nao.
Mjumuiko huo umefanyika kama sehemu ya Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya, ukutoa fursa ya kubadilisha tamaduni kupitia kioo cha jiografia kwa vitu vya asili vilivyotengezwa.