Mapinduzi ya hivi punde yalifanyika nchini Niger na Jenerali Abdourahamane Tchiani akijitangaza kama kiongozi wa nchi/ Picha: Others 

Na Abdulwasiu Hassan

Mapinduzi ya serikali nchini Niger, kufanywa na wanajeshi waliopewa jukumu la kumlinda Rais Mohamed Bazoum ,yameibua wasiwasi kuhusu kurejea tena kwa mapinduzi barani Afrika.

Kati ya 2020 na sasa, Afrika imekuwa na visa10 vya mapinduzi ya serikali viilivyokamilishwa au kutibiuka.

Nchi zilizoathirika ni pamoja na Sudan, Chad, Burkina Faso, Mali, Guinea, Guinea-Bissau, na sasa Niger.

Mkuu wa walinzi wa rais wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, alionekana kwenye televisheni ya taifa siku ya Ijumaa kama kiongozi mpya wa nchi hiyo kufuatia mapinduzi ya Jumatano.

Chanzo cha changamoto

Sababu zinazotolewa na askari hao kuchukua nafasi hiyo, zaidi ni kuhusu madai ya serikali kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Wanasema kwamba kiini cha mapinduzi kilitokana na "kuzorota kwa hali ya usalama, usimamizi mbaya wa kijamii na kiuchumi.

Haya yanaangazia hisia za wanajeshi waliofanya mapinduzi ya Agosti 2020 yaliyoiangusha serikali ya aliyekuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita.

Assimi Goïta wa Mali ameahidi uchaguzi mwaka wa 2024 /Picha: Goita Twitter         

Wale ambao waliochukua serikali ya Rais wa zamani Alpha Conde wa Guinea mwaka mmoja baadaye, mnamo 2021, walieelezea hisia sawa.

“Ukiona hali ya barabara zetu, za hospitali zetu, tambua kuwa ni wakati wa sisi kuamka,” alisema Kanali Mamady Doumbouya, aliyepindua serikali ya Conde.

Misingi ya demokrasia, kama inavyosisitizwa na wanaharakati na wanasayansi wa kisiasa, inapingana na msimamo wa pamoja wa wale waliohusika katika kupindua serikali barani Afrika.

Mahamat Deby alichukua uongozi Chad baada ya kifo cha rais Idris Deby aliyekuwa baba yake/ Picha: Getty 

"Katika siku za nyuma (miaka ya 60 hadi 80), sababu ya kawaida ambayo waliopanga mapinduzi wangetoa ni kukosekana kwa utulivu wa kisiasa na udanganyifu katika uchaguzi," alisema Dk Aminu Hayatu wa idara ya sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Bayero huko Kano, Nigeria.

"Siku hizi, hawazungumzii sana kuhusu utovu wa nidhamu katika uchaguzi. Badala yake, wanazungumzia gharama ya maisha na matatizo ambayo watu wanakabiliana nayo."

Dk Hayatu alieleza kuwa hata wale waliohusika katika mapinduzi ya serikali katika Jamhuri ya Niger hawakuhusisha vitendo vyao na udanganyifu wa uchaguzi, au mgogoro wowote wa kisiasa kama huo.

Athari kubwa zaidi

Wachambuzi wanaona kuzuka upya kwa mapinduzi ya serikali barani Afrika kama hatua ya kurudisha nyuma bara kwa miaka, ikiwa sio miongo kadhaa.

"Kama kanda ndogo, tayari kumeturudisha kutoka pale tulipokuwa miaka michache iliyopita," Idayat Hassan, mshirika mkuu katika Kituo cha Mafunzo ya Mikakati na Kimataifa, aliiambia TRT Afrika. .

Wachambuzi wanaamini njama ya mapinduzi si suluhu la haraka kwa tatizo lolote la kiuchumi.

"Magumu ambayo watu wanayakimbia yatarejea kwa sababu waliopanga mapinduzi hawana historia ya kufuata sheria zitakazohakikisha utoaji wa huduma," Dk Hayatu alisema.

"Ikiwa hali hii itaendelea katika nchi za Afrika, ukiukwaji wa haki za binadamu utaenea," alionya.

Kanali Mamady Doumbouya aliongoza mapinduzi ya serikali Guinea na kumuondoa rais Alpha konde madarakani / Photo AFP

Kwa mujibu wa Dkt. Hayatu, demokrasia inaenda sambamba na maoni ya watu, uchaguzi wa wawakilishi wa wananchi, na kufanya kazi kwa ajili ya wananchi.

"Na ikiwa utawala utaachiwa wanajeshi wachache, unajua kwamba kwa vile hawajachaguliwa, watafanya tu kile wanachopenda," alisema.

Jinsi ya kujikomboa

Kando na juhudi zinazofanywa na mashirika ya kikanda kama vile Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi kukomesha kuibuka tena kwa mapinduzi katika eneo hilo, wachambuzi wanaamini Waafrika wanahitaji kumiliki demokrasia ili kustawi.

"Mara tu wananchi wanapoacha kupigania demokrasia, dakika tu wanapoacha kuisukuma, wazo lenyewe kwa hakika liko hatarini," Hassan aliiambia TRT Afrika.

"Lazima tuwafanye wananchi kuelewa thamani ya demokrasia wenyewe. Ni lazima tuwafanye wananchi kuwa wamiliki wa demokrasia - wale ambao wataweza kulinda demokrasia yao," alisema.

Wengine wanatetea tabaka la kisiasa linahitaji kufanya kazi katika kuondoa mantiki iliyotajwa nyuma ya kila mapinduzi ya kijeshi.

Hii inajumuisha kuchukua hatua za kuondoa kutoridhika ambako wanajeshi wanaweza kutumia kama uhalali wa kushiriki katika mapinduzi.

Dkt. Hayatu anapendekeza kwamba wanasiasa wanapaswa kujifunza somo kutokana na kuzuka upya kwa mapinduzi barani Afrika.

‘’Mambo yanayotoa fursa kwa hili (mapinduzi), yakiendana na malalamiko ya askari, yana ukweli ndani yake,” alisema Dkt, Hayatu.

"Wanasiasa wanapaswa kujua hisia za raia. Ikiwa maskini hawana malalamiko haya, itakuwa vigumu kwa mapinduzi kufanikiwa."

TRT Afrika