Televisheni ya taifa nchini Mali imetangaza kuwa hali sasa imedbitiwa baada ya wapiganaji wenye silaha kulishambulia kituo cha mafunzo kwa askari katika mji mkuu wa Mali Bamako Jumanne asubuhi.
Milio ya risasi ilisikika mapema Jumanne asubuhi katika mji mkuu wa Mali Bamako. katika mtaa wa Banankabougou.
"Habari za asubuhi mabibi na mabwana, taarifa hizi zimetufikia hivi punde, asubuhi ya leo kundi la magaidi limevamia shule ya kikosi cha usalama cha Faladie , shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo lote. Hali imedhibitiwa," taarifa katika televisheni ya taifa ilisema.
" Tunaomba wenyeji wa eneo hilo kuwa watulivu na kufuata maagizo yaliyotolewa na vikosi vya usalama na kukaa karibu kupata habari rasmi inapopatikana," taarifa hiyo iliongezea.
Watu waliokuwa wakielekea msikitini kuswali sala ya asubuhi walilazimika kurudi huku milio ya risasi ikivuma.
Walioshuhudia waliambia sirika la Reuters kuwa milio ya risasi ilianza karibu saa Kumi na moja alfajiri.
Baadhi ya wakazi walisema ilitoka upande wa uwanja wa ndege,