Waandamanaji wamelaani shambulio la PKK ambalo limeuwa wanajeshi 12 wa Uturuki kaskazini mwa Iraq wiki kadhaa zilizopita. / Picha: AA  

Mamia kwa maelfu ya watu wamekusanyika katika tukio lililoitwa, "Huruma kwa Mashahidi wetu waliokufa, kuunga mkono Palestina, laana kwa Israeli" katika misikiti baada ya swala ya alfajiri ili kushiriki katika msafara ulioratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Uturuki TUGVA na Jukwaa la Utashi wa Kitaifa-National Will Platform.

Shughuli hiyo ilikuwa na ushiriki wa taasisi zisizo za kiserikali 308 (NGOs). Baada ya swala ya alfajiri, katika misikiti ya Hagia Sophia, Eminonu, Sultanahmet, na Suleymaniye siku ya Jumatatu, washiriki walikusanyika katika viwanja vya misikiti, wakiwaombea mashahidi waliouawa na Wapalestina ambao wamepoteza maisha yao kutokana na mashambulizi ya Israeli.

Washiriki walikusanyika katika Uwanja wa Hagia Sophia Square baada ya swala ya alfajiri na kuimba nyimbo kama, "Mashahidi hawafi kamwe, nyumbani hakutagawanyika," "Wanaoshirikiana na wasaliti watahukumiwa, muuaji Israeli atahukumiwa," "Muuaji Israeli, toka Palestina," "Damu yetu, maisha yetu yanajitolea kwa Al Aqsa," na "Salam kwa Hamas, ukakamavu utaendelea."

Waziri wa Vijana na Michezo, Osman Askin Bak, aliyekuwa spika wa Bunge la Uturuki Mustafa Sentop, na rais wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Usambazaji Elimu na mjumbe wa Bodi ya Juu ya Ushauri ya TUGVA, Bilal Erdogan, walikuwa miongoni mwa walioshiriki.

Maombi pia yalifanywa kwa wanajeshi 12 wa Uturuki waliouawa katika oparesheni iliyopewa jina la Claw-Lock Operation kaskazini mwa Iraq na wale waliouliwa kutokana na mashambulizi ya Israeli huko Gaza.

Baada ya dua, washiriki hao walianza kutembea kuelekea Daraja la Galata, wakibeba vipeperushi vyenye ujumbe kwa lugha ya Kituruki, Kiarabu na Kiengereza.

TRT World