Vijana walijipanga kunadamana Kampala Mjii Mkuu wa Uganda | Picha AFP

Mamlaka nchini Uganda zilipanga jeshi na polisi Jumanne kuzunguka bunge na maeneo mbali mbali ya Kampala, mji mkuu, kwa lengo la kuzuia maandamano dhidi ya serikali yaliyopangwa na vijana.

Magari ya kivita ya jeshi yalikuwa yakizunguka mitaa kuzunguka bunge katika picha zilizorushwa na televisheni ya NTV Uganda baada ya polisi kupiga marufuku maandamano hayo, wakisema intelijensia inaonyesha kuwa vijana wenye nia ya uhalifu wanaweza kuyateka kwa ajili ya kupora na kuharibu mali.

Barabara zote kuelekea bungeni zilifungwa, huku maafisa wa usalama wakiruhusu tu wabunge na wafanyakazi wengine wa bunge kupita.

Wale wenye biashara karibu na bunge walikuwa wakipata ugumu kufika kwenye majengo yao, shahidi wa Reuters alisema.

Kukataa marufuku

"Ni kama eneo la vita," Edwin Mugisha, ambaye anafanya kazi Kampala, aliiambia Reuters, akielezea doria kuzunguka bunge na barabara nyingine.

Kumekuwa na ripoti kwamba vikundi vidogo vya waandamanaji vilijitokeza Kampala licha ya marufuku ya maandamano.

Vikosi vya usalama vya Uganda vilikamata baadhi ya vijana katikati mwa Kampala ambao walikuwa wakishiriki katika maandamano yaliyopigwa marufuku.

Shahidi wa Reuters aliona watu wakikamatwa, wakati video iliyorushwa na NTV Uganda kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii la X pia ilionyesha kundi dogo la vijana likikamatwa na polisi walipokuwa wakiandamana.

Mjadala wa mashtaka

Jumatatu polisi walifunga ofisi za chama kikuu cha upinzani, wakikilaumu kwa kuandaa maandamano, na kuwakamata baadhi ya maafisa wa chama, wakiwemo wabunge wake.

Chama hicho kilikanusha kuwa kilikuwa kinaandaa maandamano hayo, lakini kilisema kinaunga mkono.

Viongozi wa upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu wamekuwa wakimtuhumu Rais Museveni kwa kushindwa kuwafikisha mahakamani maafisa wakuu waliorubuni.

Museveni amekana mara kwa mara kuruhusu ufisadi na kusema kila inapokuwa na ushahidi wa kutosha wahusika wanachukuliwa hatua, kama vile wabunge na hata mawaziri.

Reuters